Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kushoto)
akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi Kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw.Denis Daudi, wakati alipokagua
huduma za mabasi katika kituo cha nane nane Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
Kushoto), akikagua moja ya kifaa kinachotumika kwenye Reli wakati
alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA),
Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto) akikata moja ya kifaa kinachotumika kujengea reli wakati
alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro
Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishiriki
kuweka zege kwenye mashine ya kutengenezea mataruma ya Reli wakati
alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro
Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
Mkoa wa Tanzania Bw. Fuadi Abdallah wakati alipokagua Mtambo wa kupimia
ubora wa vifaa vya ujenzi katika Kiwanda hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua moja
ya kifaa cha kutengenezea Mataluma wakati alipokagua kiwanda cha
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani
Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
Watendaji na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara yake (hawapo
pichani) wakati alipokutana nao Mkoani Mbeya.
Watendaji
na wafanyakazi wa taasisi zilizopo chini ya Wizara yake wakimsikiliza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo
pichani), wakati alipozungumza nao Mkoani Mbeya.
Serikali
imesema itatumia kiwanda cha Kongolo cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA) kilichopo Mbeya kuzalisha mataruma yatakayotumika
kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) inayotarajiwa kuanza
kujengwa hivi karibuni ili kupunguza gharama.
Hayo
ameyasema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa alipotembelea kiwanda hicho kuona utendaji kazi na uzalishaji
unaopatikana na kuiagiza kamati maalumu ya ujenzi wa reli hiyo
kutembelea kiwandani hapo kuangalia uwezo wa uzalishaji wa kiwanda
hicho.
Profesa
Mbarawa amesema Serikali ina dhamira ya kufufua viwanda hapa nchini ili
kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania na kuifikisha nchi katika uchumi
wa kati kupitia mapinduzi ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
"Nitahakikisha
mkandarasi atakeyejenga reli hii anatumia mataruma yatakayozalishwa
katika kiwanda hiki, badala ya kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nchi za
nje", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa kwa kutumia kiwanda hicho Serikali itaokoa pesa ambazo zitaisaidia
TAZARA kujiongezea mapato yatakayotokana na matengenezo ya mataruma na
kupanua wigo wa kibiashara kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amekagua maabara ya kupima viwango na ubora wa
kokoto na nondo kilichopo kiwandani hapo na kutoa mwezi mmoja kwa
TAZARA kupata cheti cha ukaguzi kutoka Shirika La Viwango (TBS), ili
iweze kurasimishwa rasmi.
Kwa
upande wake Msimamizi Mkuu wa kuzalisha mataruma katika Kiwanda Cha
Kongolo cha TAZARA-Mbeya Eng. Boniface Phiri amesema kuwa fursa ya kuwa
sehemu ya mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa itaongeza uzalishaji wa
kiwanda na kukuza pato la Mamlaka. "Kwa kushirikiana na wenzetu
tutaongeza vifaa ili tuweze kuzalisha kwa wingi na ubora unaotakiwa
katika mradi huu", amesema Eng. Phiri.
Kiwanda
cha Kongolo ni kiwanda pekee katika nchi za Afrika na kati
kinachozalisha mataruma kwa ajili ya reli na kina uwezo wa kuzalisha
mataruma elfu ishirini na nne kwa mwaka. Waziri Prof. Mbarawa yupo
katika ziara ya kukagua miundombinu ya reli, barabara na mawasiliano
mkoani Mbeya.


0 comments:
Post a Comment