https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    FC BARCELONA VS ATLETICO MADRID; ‘ NI UFUNDI DHIDI YA MBINU, ENLIQUE & SIMEONE….

    Atletico Madrid ilitwaa ubingwa wa La Liga, Mei 17, 2014 baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na FC Barcelona katika siku ya mwisho ya msimu ndani ya uwanja wa Nou Camp. Lilikuwa taji la kwanza kwa timu hiyo ya Madrid tangu mwaka 1996. Ilikuwa ni zawadi nzuri ambayo mlinzi Diego Godin aliitoa kwa klabu yake na kocha Diego Simeone baada ya kuruka juu kiufundi na kufunga kwa kichwa bao muhimu zaidi kwa timu yake msimu uliopita.
    Ikihitaji ushindi tu katika uwanja wa nyumbani ili kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, mshambulizi Alwx Sanchez aliifungia Barca bao la kuongoza katika dakika ya 33 na kudumu hadi nusu ya kwanza ya mchezo kabla ya Godin kufunga la kusawazisha dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili katika mchezo ambao ulitoa kadi nane za njano
    barca
    Timu hizo mbili zinakutana katika pambano la raundi ya 18 saa tano usiku kwa masaa ya Afrika
    Mashariki. Barca iliyo katika nafasi ya pili itacheza na Atletico iliyo nafasi ya tatu katika uwana wa Nou Camp. Timu zote zinawania kupunguza ‘ gepu; la pointi dhidi ya viongozi Real Madrid ambao waliishinda Espanyol kwa mabao 3-0 jana Jumamosi. Real iko mbele kwa tofauti ya pointi nne licha ya tofauti hiyo kupungua Baada ya mchezo wa Barca na Atletico ambazo zote zina pointi 38.
    Katika safari tatu zilizopita katika dimba la Camp Nou, Atletico haijapoteza mchezo. Imefanikiwa kufunga mara mbili na kuruhusu mabao mawili katika michezo mitatu ya michuano tofauti. Luis Enlique mkufunzi wa Barca anataraji kuwaanzisha washambuliaji wake watatu wa ‘ Ki-Amerika, Leonel Messi, Neymar Da Silva na ‘ mtukutu’ Luis Suarez licha ya watatu hao kushindwa kutoa matunda mazuri. Labda mechi hii inamuhitaji mchezaji mwenye ujanja, kasi na nguvu, Pedro Rodriguez katika wingi ya kulia.
    Messi amefunga mabao 15 hadi sasa katika La Liga, wakati Neymar tayari amemudu kufunga mabao 11. Atletico walifunga mabao mawili dhidi ya Real Madrid mapema wiki hii baada ya walinzi wa Real kulazimishwa kufanya makosa. Godin, Jose Gimenez, Lucas Fernandez na Jesus Gamez waliibana safu kali ya mashambulizi ya Real hivyo ili kuweza kuvunja ukuta huo na kumfikia kipa, Jan Oblak itamlaimu Enrique kumpanga Pedro ambaye jujibadilisha na kuwa kiungo, mshambuiaji na kusaidia ulinzi kila eneo analokuwepo.
    Atletico ni timu ngumu sana, ina ‘ piga viatu’ huku wachezaji wake wa kati wakicheza kwa nguvu kila wanapokutana na Barca. Mario Suarez, Gabriel Fernandez ‘ Gabi’, Saul Niguez walicheza vizuri dhidi ya Real katika eneo la katikati ya uwanja. Lakini Simione atawarudisha kikosi cha kwanza Tiago Mendez, Arda Turan na Koke ambao katika michezo mitatu ya mwisho msimu ulipita watatu hao walikuwa ‘ sumu’ kwa safu ya kiungo ya Barca.
    Baada ya mchezo huo Messi atakwenda Zurich, Uswisi katika tuzo za mwanasoka bora wa dunia na wakati mpinzani wake mkubwa katika tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo akinza bila mabao mwaka mpya, Messi anaweza kuzima kelele zote kuwa ataondoka ndani ya Barca. Hii ni mechi ambayo inawajitaji wachezaji wakubwa ili watuoneshe ubora wao. Ninge,uanzisha nje Suarez na kumpanga Pedro ‘ laiti’ ningekuwa katika nafasi ya Luis. Pedro ni mchezaji anayeweza kunipa kasi akitokea pembeni sehemu ambayo mara nyingi hushirikiana na Dan Alves.
    Katika mchezo waliopoteza dhidi ya Real Sociedad wiki iliyopita, Enlique aliwapanga Jeremy Mathieu, Javier Mascherano, Jordi Alba na Martin Montoya katika safu ya ulinzi, Sergio Busquets, Andres Inesta na Xavi Hernandez walianza katika eneo la kiungo na timu ilimiki mchezo kwa asilimia 73. Kama Enlique atawaamini viungo hao kwa mara nyingine anaweza kupata ushindi, lakini wasiwasi mkubwa unabaki katika ‘ nyuza zilizopo katika ngome’.
    Fernando Torres ataanza kwa mara nyingine baada ya kucheza kwa dakika 59 dhidi ya Real, Mario Mandzukic aliingia kuchukua nafasi ya Antonie Griezmann na kucheza kwa muda war obo saa katikati ya wiki anaweza kuanza safari hii katika uwanja wa Camp Noun a bila shaka Barca wanakumbuka namna alivyowatenda katika mipambano ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa miaka miwili iliyopita alipokuwa akiichezea FC Bayern Munich ya Ujerumani.
    Hii ni mechi ambayo inawakutanisha mabingwa watetezi na makamu bingwa wake. Si ya kukosa. Je, mshindi nani?
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FC BARCELONA VS ATLETICO MADRID; ‘ NI UFUNDI DHIDI YA MBINU, ENLIQUE & SIMEONE…. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top