https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Gazeti la The EastAfrican lapigwa marufuku Tanzania



     


    Gazeti la The EastAfrican lapigwa marufuku Tanzania
    Serikali ya Tanzania imepiga marufuku kuchapishwa na kusambazwa kwa gazeti la kila wiki la The EastAfrican kwa madai ya kuwa halijasajiliwa nchini humo.

    Hata hivyo Wilfred Kiboro, mwenyekiti wa kampuni ya Nation Media Group, wachapishaji wa gazeti hilo la lugha ya kiingereza, ameeleza kuwa adhabu hiyo haikutarajiwa na wala haistahili na kubainisha kuwa wamekuwa wakisambaza gazeti hilo Tanzania kwa miaka 20 bila matatizo.
    Kampuni ya Nation imedai sababu kubwa huenda ni serikali ya Tanzania kutofurahishwa na msimamo wake wa kuandika habari dhidi ya maovu kama rushwa na kero nyingine nchini Tanzania.
    Kampuni hiyo imesema serikali ya Tanzania imetaja kutofurahishwa na kibonzo kilichochapishwa katika toleo la wiki hii, ambapo imesema kimemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Gazeti la The EastAfrican lapigwa marufuku Tanzania Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top