
Wakati
mambo yakionekana kana kwamba yameanza kumnyookea, kocha mpya wa klabu
ya Real Sociedad, Mscotish David Moyes baada ya kupata ushindi mbele ya
klabu ya Fc Barcelona sasa mambo yanaonekana kugeuka na kurejea kulekule
kwenye ugumu.
Meneja
huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United alitolewa kwa kadi
nyekundu kwenye mchezo wa timu yake ya Real Sociedad dhidi ya nyambizi
wa Villarreal kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Copa Del
Rey usiku wa jana.
Moyes
hakuonekana kujali kadi hiyo kwani mara baada ya kutoka benchini na
kwenda kukaa jukwaani aliamua kuanza kugonga vitafunwa vilivyokua
vikiliwa na mashabiki waliokuwa wamekaa uwanjani hapo huku akionesha
tabasamu zito kwa mashabiki hao.

