
KIPINDI cha usajili kwa Ligi Kuu Bara ni kipindi cha vituko. Mambo mengi ya kushangaza, visa na vitimbi vingi hutokea kipindi hiki hususan kwa timu za Simba na Yanga.
Wachezaji ambao hata usiowadhania husajiliwa na
klabu hizi, kwa njia sahihi ama kwa visa na fitina. Ni kipindi ambacho
Simba na Yanga hutambiana katika idara tofauti, kila timu huonyesha
ubabe wake.
Ubabe na tambo hizi za Simba na Yanga
zimesababisha timu hizi kufanya baadhi ya maamuzi ya kishabiki. Wamekuwa
wakisajili ama kuwaachana baadhi ya wachezaji bila sababu za msingi.
Mwanaspoti inakuletea orodha ya mastaa ambao Simba
na Yanga ziliachana nao kimakosa. Timu hizi zilipaswa kufanya jitihada
binafasi kuwabakisha klabuni hapo kutokana na umuhimu wao.
Frank Domayo, Yanga
Yanga ilikosea kuachana na kiungo, Frank Domayo
wakati akiwa kwenye ubora wake. Domayo, 22 aliondoka Yanga baada ya
mkataba wake kumalizika msimu uliopita na kuamua kujiunga na Azam FC.
Wakati Domayo anaondoka Yanga, alikuwa kwenye
kiwango cha juu na hata alipoondoka pengo lake lilionekana katika kikosi
hicho. Licha ya kukaa nje kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji
nchini Afrika Kusini mapema mwezi Julai mwaka jana bado nafasi yake pale
Yanga ilikuwa wazi.
Domayo amerejea uwanjani kwa sasa na Jumanne ya
wiki hii aliichezea Azam mechi yake ya kwanza ya mashindano na kuonyesha
kiwango cha juu kilichomshtua kocha wa timu hiyo, Joseph Omog raia wa
Cameroon.
Didier Kavumbagu, Yanga
Hapa Yanga ilibugi zaidi. Iliamua kuachana na
mshambuliaji Didier Kavumbagu baada ya kumalizika kwa msimu uliopita
wakati straika huyo akiwa bado moto. Yanga haikuonyesha jitihada zozote
za kuongeza mkataba wa
Hapa majibu hakuna. Kulikuwa na sababu gani ya Yanga kuachana na
mshambuliaji Hamis Kiiza raia wa Uganda? Ni siasa tu. Kiiza aliifungia
timu hiyo mabao 11 msimu uliopita huku akitengeneza mengine zaidi ya 10.
Hakukuwa na swali juu ya kiwango cha mshambuliaji huyo.
Tatizo lilianza pale Kocha Mbrazili Marcio Maximo
alipopewa kazi ya kuifundisha timu hiyo, kwani alipendelea zaidi
kuwatumia viungo ili kucheza soka la kujilinda jambo lililofanya Kiiza
aonekane si lolote kwenye kikosi hicho na baadaye Yanga kuamua kuachana
naye kwenye usajili wa dirisha dogo. Hapa Yanga ilibugi. Hakukuwa na
haja ya kumwacha Kiiza na kuhangaika kutafuta washambuliaji wengine
hususan timu ilipoamua na kuachana na Maximo.
David Luhende, Yanga
Hapa Yanga ilikosea zaidi. Timu hiyo iliamua
kuachana na beki wake wa kushoto David Luhende kwa sababu tu za kisiasa
wakati kiwango chake uwanjani kilikuwa juu. Baada ya Yanga kuachana na
Luhende iligundua kuwa haina beki mwingine wa kushoto wa kusaidiana na
Oscar Joshua. Hapa Yanga ikaamua kumsajili beki wa JKT Ruvu, Edward
Manyama ambaye ameshindwa kufiti moja kwa moja kwenye kikosi hicho.
Luhende aliamua kujiunga na Mtibwa Sugar ya
Morogoro na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu
hiyo. Hakika Yanga ilibugi na sasa inahaha tu kwani kiwango cha Oscar
nacho ni cha kawaida mno.
Amissi Tambwe, Simba
Simba hapa ilibugi pengine zaidi ya timu zote
baada ya kuamua kuachana na straika Mrundi Amissi Tambwe. Straika huyo
aliibuka mfungaji bora wa msimu uliopita akiwa amefunga mabao 19 (tisa
ya penalti) lakini baada ya mechi saba tu za msimu huu timu hiyo iliamua
kumfungulia mlango wa kutokea. Aliyekuwa Kocha wa Simba, Patrick Phiri
raia wa Zambia alidai kuwa Tambwe hawezi kufanya vizuri kwenye mfumo
wake hivyo kuishia kumweka benchi.
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga kwenye pambano
la Mtani Jembe huku Tambwe akiwa benchi, ulionekana kuwapa kiburi watu
wa Simba na kuamua kuachana na straika huyo ambaye alitua Yanga saa
chache baadaye. Tambwe tayari ameifungia Yanga bao moja katika mechi
tatu alizocheza huku akionekana kuwa na uchu wa kufunga zaidi na zaidi.
Hapa Simba walibugi.
Kelvin Yondani, Simba
Beki Kelvin Yondani alimaliza mkataba wake na
Simba baada ya kumalizika kwa msimu wa 2011/12 huku timu hiyo ikionekana
kuwa kimya. Baada ya mazungumzo, viongozi wa Simba walimpa ahadi ya
kumpatia mkataba mpya punde kabla ya msimu mpya kuanza.
Baada ya Yondani kuona Simba haina dhamira ya
kumpatia mkataba mpya aliamua kujiunga na Yanga. Hapa Simba ilikurupuka
kwani baada ya kuondoka kwa Yondani mambo yalionekana kwenda ndivyo
sivyo kikosini hapo. Hali ilikuwa mbaya zaidi kwani mbali na kuondoka
kwa Yondani, timu hiyo pia ilimwondoa beki Juma Nyosso na kuifanya beki
ya kati ya timu hiyo kuwa uchochoro.
Pengo la Yondani limeendelea kuitesa Simba hadi
sasa kwani baada ya kuondoka tayari mabeki zaidi ya wanne wamesajiliwa
na kushindwa kuziba nafasi hiyo wakati Yondani ameendelea kuwa msaada
mkubwa kwenye kikosi cha Yanga.
credit mwana spoti
Salum Kanoni, Simba
Simba iliamua kuachana na beki wa kulia Salum
Kanoni mwaka 2012 baada ya Said Nassoro ‘Chollo’ kuonyesha kiwango cha
juu kikosini hapo. Simba haikuona umuhimu wa kuwa na Kanoni wakati
Chollo tayari amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Hilo lilikuwa ni tatizo kwani hali ilibadilika
baadaye kwani Chollo alikosa mpinzani wa kiwango chake na alipoanza
kusumbuliwa na majeraha eneo la beki hiyo ya kulia liligeuka kuwa
uchochoro. Simba ikaanza kuhaha kutafuta beki mwingine wa kuziba nafasi
hiyo.
Msimu huu imemsajili Hassan Kessy kutoka Mtibwa
Sugar kwa Sh 30 milioni pamoja na kumtoa beki Miraji Adam akacheze kwa
mkopo klabuni hapo kama sehemu ya uhamisho huo. Kanoni bado ameendelea
kutamba ligi kuu akiwa na kikosi cha Kagera Sugar huku baadhi ya
viongozi wa Simba wakionekana kummezea mate.
Juma Kaseja, Simba
Yawezekana Simba walikuwa na hoja juu ya kipa Juma
Kaseja lakini haikuwa wakati muafaka kuachana naye. Kwa kifupi ni
kwamba walistahili kuachana naye lakini hawakujiandaa kwa ajili ya hilo.
Ilikuwa hivi, Simba iligoma kumwongezea mkataba Kaseja baada ya ule wa
awali kumalizika baada ya msimu wa 2012/13 na kuamua kumsajili kipa
Mganda Abel Dhaira ili kuziba pengo lake.
Hapa walibugi. Dhaira alikuja na kucheza kwa nusu
msimu pekee. Kiwango chake kilionekana kuwa duni. Baada ya kuachana na
kipa huyo Simba iliamua kuwasajili makipa wa zamani wa Yanga, Yaw Berko
na Ivo Mapunda ili kuimarisha lango lao jambo ambalo limeonekana pia
kufeli. Berko alichemka na kuondoka tu baada ya nusu msimu,
Mapunda amekuwa akilaumiwa kuwa anafungwa mabao
mepesi. Viongozi wa Simba wenyewe wanajua kuwa walibugi kuachana na
Kaseja. Kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi uliopita viongozi wa Simba
walipambana kumrejesha Kaseja lakini jitihada zao ziligonga mwamba
kutokana na kuwa na mkataba na Yanga.
credit mwana spoti

