Mbwa
mmoja wa Polisi huko New Jersey Marekani mwenye umri wa miaka nane
aliyefanya kazi kwa miaka minne amelazimika kustaafu kutokana na afya
yake kuwa mbaya.Mbwa huyo wa Polisi ambaye anaitwa Judge amepewa heshima
na kuagwa kishujaa, kaandaliwa na gwaride pamoja na kupigiwa saluti na
Polisi tukio ambalo lilishuhudiwa pia watu wa haki za wanyama.
Judge
alikuwa anastaafu kama mbwa wa Polisi huko West Deptford Township,
ambapo alitakiwa kustaafu tangu mwaka 2013, kutokana na maradhi ya meno
na pia afya yake ilianza kuzorota kwa kasi.Tangu ameanza kuumwa 2013
hali ya afya yake haikuwahi kuwa nzuri, watu wa haki za wanyama waliona
ni vizuri ‘astaafishwe’ na pia wakashauri aendelee kupatiwa matibabu
katika Hospitali ya wanyama ya Swedesboro.
Huu ni msafara wa gari zilizombeba mbwa huyo.
Tukio hilo sio geni sana kwa wenzetu, kuliwahi kuwa na story ya ishu ya mbwa mmoja wa Polisi ambaye alizikwa kwa heshima kama ambavyo huwa mazishi ya askari yanafanyika.Angalia picha hapa chini
Shughuli za mazishi ya mbwa.