Mfanyakazi wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited Patrick
Pera, akionyesha mkono uliopigwa risasi akiwa katika hospital ya Amana
jijini Dar es Salaam Watu wasiojulikana wamempiga risasi moja ya mkono
na kumpora fedha kiasi cha Sh2milioni mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi
Communication Limited, Patrick Pera mara baada ya kutoka kuzichukua
katika benki ya NMB tawi la Mandela jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea leo mchana katika kituo cha mafuta cha Oil Com
kilichopo katika eneo la Tabata Relini wakati Pera alipokuwa amepakia
kwenye pikipiki huku akiwa na idadi hiyo ya fedha kutoka benki
Akizungumza na tovuti hii akiwa katika hospital ya Amana jijini Dar
es Salaam kabla ya kuhamishiwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili,
Pera ambaye ni Mhariri msaidizi wa habari za kwenye mtandao amesema
alifika katika benki hiyo majira ya saa nane ili kuchukua kiasi hicho
cha fedha kwa ajili ya matumizi muhimu.
Amesema baada ya kuandikisha fomu na kupatiwa fedha hizo alitoka nje
ya benki hiyo na moja kwa moja alielekea kwa waendesha pikipiki maarufu
kama bodaboda ili kukodi kwa lengo la kuletwa ofisini kabla ya kwenda
kukabidhi fedha hizo kwa kaka yake.
Amesema waendesha bodaboda walianza kutupiana mpira huku kila mmoja
akitaka mwenzake ampeleke ndipo kijana mmoja alipoamua kumpakia.
Amesema kabla ya kufika ofisi za MCL wakiwa kwenye kituo cha mafuta
cha OIL Com walitokea vijana wengine wawili waliokuwa na pikipiki na
kumuamrisha atoe fedha alizokuwa nazo.
Amesema aliwauliza kuwa wao ni wakina nani, ndipo walipomuonyesha
bastola na akaamua kuwapatia fedha hizo, lakini kama hiyo haitoshi
wakaamua kumpiga risasi moja mkononi.
Tovuti ya mwananchi iliyokuwepo katika hospitali ya amana iliambiwa
kuwa risasi iliyopigwa mkononi mwa Pera imesaga mfupa hivyo anahamishiwa
kwenye Hospital ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa
hospital hiyo haina uwezo wa kufanya hivyo.
Aidha Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
uchunguzi umeanza mara moja kwa kumshikilia na kumuhoji kijana wa
Bodaboda aliyekuwa anamuendesha Pera alipokuwa akitokea benk