Baadhi
ya Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza
lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa
mstaafu wa jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
Ndugu
wa marehemu akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi
wakati wa Kutoa Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa
Mzee Andrew Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea
tarehe 14 Februari 2015.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon
Siro akitoa maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu
Mzee Andrew Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew
Kumalilwa alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake
Tabata Segerea.
Jeneza
lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari
kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na
kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili
wake katika Nyumba yake ya Milele.
Askari
wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa
aliyekuwa DCP Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael
Kumalilwa wakiingia katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili
ya Misa na ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya
kwenda kuupumzisha katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa
katika nyumba kwake Tabata Segerea.
Mtoto
wa Kwanza wa Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa
mwenye huzuni wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu
alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
Jeneza
lililokuwa limebeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa
ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya kuelekea
nyumbani Kwake Segerea ambapo mazishi yalifanyika.