Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Alphayo Kidata
(kulia) bakitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu
linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni jana jijini la Dar es
salaam.Kulia ni Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidata (hayupo pichani) alipokuwa
akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo
yanayomilikiwa kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni
jana jijini Dar es salaam.
Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana.
Baadhi
ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika
maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia
maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.
Fundi
wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na zoezi la
kukata umeme eneo la Mikocheni B kufuatia zoezi la bomoa bomoa
lililokuwa likiendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi na Manispaa ya Kinondoni, jana jijini Dar es salaam.
Tingatinga
likiendelea kubomoa maduka eneo la Tegeta Machakani kufuatia maduka
hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.
Askari
wa Jeshi la Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa zoezi la bomoa
bomoa maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kinyume cha sheria kutoka
kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali eneo la Mikocheni na Tegeta jijini
Dar es salaam.