Mkurugenzi
wa Habari Elimu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisogwa
(katikati) akizungumza jambo, kulia ni Afisa Mwandamizi wa Elimu Bodi ya
Elimu ya Juu, Veneranda
Malima na kushoto ni Juma Chagonja, Mkurugenzi
wa Urejeshaji Mikopo ya Elimu ya Juu.
Viongozi hao wa Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu wakiandika maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
BODI ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
imetoa ufafanuzi juu ya namna ambavyo wanatekeleza majukumu yao ya
kutoa na kurejesha mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema
leo hii katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Mkurugenzi wa Habari
Elimu wa Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisogwa alisema tangu
bodi hiyo ilipoanzishwa mwaka 2005, pamoja na utekelezaji wa sera ya
uchangiaji, ilipewa majukumu mawili makubwa, kutoa mikopo kwa wanafunzi
wahitaji na kurejesha mikopo ya elimu kuwa endelevu.
Alisema kampeni ya urejeshwaji wa mikopo
hiyo iliyoanza rasmi mwaka 2006/2007, imekuwa na mafanikio makubwa
katika ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika wa mikopo.
Mwaisogwa alibainisha baadhi ya mikopo ya
fedha iliyotolewa kwa mwaka 1994/1995 kuwa ni Sh. 1,807,223,411,221.00
ambapo Juni, 2014 kati ya hizo, Sh.51,103,685,914 zilitolewa na
iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na kiasi
kilichobaki cha Sh. 1,756,119,725, 307.00 kilitolewa na bodi ya mikopo
tangu Julai, 2005 bodi hiyo ilipoanza kazi rasmi.
Aliongeza kuwa, hadi sasa mikopo yote
iliyotolewa na bodi hiyo kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995 inabeba tozo
la utunzaji wa thamani ya mikopo (value retention fee) kwa asilimia 6
kwa mwaka, kwa kiasi chote ambacho hakijarejeshwa.
Alisema bado kuna wadau wenye imani potofu kuwa fedha hizo zinazotolewa ni ruzuku.
“Imani hiyo potofu inazorotesha juhudi za ukusanyaji wa madeni na inachangia ongezeko la waombaji wa mikopo hata wale ambao wana uwezo wa kujigharamia,” alisema Mwaisogwa na kuongeza:
“Imani hiyo potofu inazorotesha juhudi za ukusanyaji wa madeni na inachangia ongezeko la waombaji wa mikopo hata wale ambao wana uwezo wa kujigharamia,” alisema Mwaisogwa na kuongeza:
“Mikopo hiyo inatakiwa kurejeshwa mwaka
mmoja baadaye baada ya kuhitimu masomo. Endapo mwanafunzi akikatisha
masomo, atalazimika kurejesha mkopo huo palepale.”