https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MAAJABU 7 MAZITO ALIYETILEWA VYUMA TUMBONI MUHIMBILI


    KWELI ni maajabu! Yule mgonjwa ambaye mpaka sasa, madaktari hawataki kumtaja jina, aliyelazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Dar baada ya kufanyiwa
    upasuaji na kutolewa rundo la vyuma tumboni, maajabu saba yameibuka, Uwazi  linakupa zaidi.
    Tukio hilo la kihistoria lilitokea wiki iliyopita  ambapo mgonjwa huyo alifikishwa Muhimbili akitokea Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
    Mgonjwa ambaye mpaka sasa, madaktari hawataki kumtaja jina, aliyelazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Dar baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa rundo la vyuma tumboni.
    Kwa mujibu wa ndugu mmoja ambaye hakupenda jina lake lichapwe gazetini, vyuma mbalimbali vilivyotolewa tumboni kwa mgonjwa huyo vinaunga moja kwa moja na mambo ya ushirikina.

    AJABU NAMBA MOJA
    Ndugu huyo alisema kuwa, mgonjwa wake alikuwa akienda chooni bila shida ambapo baada ya kutolewa vitu hivyo, wengi  walitarajia alikuwa hapati choo jambo ambalo si la kweli.
    Rundo la vyuma vilivyotolewa tumboni madaktari.
    AJABU NAMBA MBILI
    “Kuna sauti ya mwanamke ilikuwa ikimwita mara kwa mara bila kujulikana ni nani wala kuonekana. Ndiyo maana tunaamini kuwa, vitu vile kuwa tumboni mwake kulitokana na mambo ya kishirikina,” alisema ndugu huyo.

    AJABU NAMBA TATU
    Ilielezwa na ndugu huyo kwamba, kabla mgonjwa huyo hajajulikana ana matatizo gani alikuwa akisikia uzito mkubwa ndani ya tumbo hali iliyokuwa ikimfanya ahisi amebeba zigo f’lani.
    “Yeye mwenyewe alikuwa akisema ana kitu tumboni, aliamini ana uvimbe mkubwa sana kwani ulikuwa ukitikisika wakati wa kutembea lakini kudhani ni vyuma, wala,” alisema ndugu huyo.
    Afisa Uhusiano Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligalesha akiangalia vyuma hivyo.
    AJABU NAMBA NNE
    Katika hali ya kushangaza, mgonjwa huyo aliweza kula ugali kiasi kikubwa sana licha ya tumboni mwake kuwa na mzigo mkubwa wa vyuma.

    AJABU YA TANO
    “Kuna mzee mmoja kule Kibaha anakoishi alikuwa akimwambia mara kwa mara kwamba anatakiwa kwenda hospitali kupima afya yake kwani mwonekano wake ulikuwa ukitoa tafsiri kwamba, ndani ya mwili wake si kuzuri lakini alikuwa akipuuzia kwa kuamini hali aliyonayo angepona kawaida tu. Ni ajabu sana, sijui yule mzee alikuwa akimwonaje?” alisema ndugu huyo.

    AJABU NAMBA SITA
    Ndugu: “Kikubwa ni kwamba, licha ya mzigo wote ule wa vyuma kuwepo tumboni, lakini alikuwa akipata usingizi kama kawaida. Na ilikuwa ili apate usingizi lazima alale chali (kuangalia juu).
    “Hapo usingizi ni mpaka asubuhi. Lakini kusema ukweli kwa mzigo ule wa vyuma tumboni bado ni ajabu, ilitakiwa asilale kabisa.”
    Akiendelea kufanya uchunguzi wake.
    AJABU NAMBA 7
    Hili ndilo ajabu kubwa kuliko yote, kwani ndugu huyo alisema mpaka sasa anashindwa kufahamu vyuma vile viliingiaje ndani ya tumbo la mgonjwa huyo kwa vile, vyuma hivyo vingi haviwezi kupita kwenye koo kwenda tumboni.

    ALIFIKAJE MUHIMBILI
    Ndugu huyo alisema kuwa, mgonjwa wake alikuwa akitumia dawa za asili Kibaha lakini hali ilivyozidi kuwa mbaya, aliamua mwenyewe kwenda Hospitali ya Tumbi na baadaye Muhimbili.
    “Alipofika Tumbi madaktari walimshauri aje Muhimbili kwa uchunguzi na kisha matibabu. Baada ya kufika alifanyiwa  uchunguzi wa kina kwa kupigwa X-ray haraka ambapo alibainika ana tatizo  kubwa tumboni na kuwalazimu  kumfanyia upasuaji.

    Bado madaktari wa Muhimbili wanashangazwa na wingi wa vyuma walivyovikuta ndani ya tumbo la mgonjwa huyo na jinsi ilivyoingia, kwani ni sayansi nyingine kabisa.

    KILICHOKUTWA
    Vyuma vilivyokutwa ndani ya tumbo la mgonjwa huyo ni misumari, bisibisi, nondo iliyopinda, plagi ya gari, mkufu na kanda ndefu ya kaseti.
    Vyuma vingine ni vipande vya mawe, pini, funguo za vitasa vya milango ya nyumba, kasha ya risasi na kifaa cha kubania wembe kwa vinyozi.
    Afisa Uhusiano Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligalesha alisema mgonjwa huyo jina lake  linaendelea kuhifadhiwa na kukiri alifika hapo wiki tatu zilizopita akitokea Tumbi.
    “Ndugu waandishi kama mnavyoona, mgonjwa  huyu alikuwa  na taizo  kubwa  si  jambo la kawaida  mwanadamu  kuishi na vyuma tumboni. Upasuaji wake ulichukua saa mbili na nusu,” alisema  msemaji huyo.
    Naye mganga wa tiba ya kienyeji, maarufu maeneo ya Kigogo, Dar alipoulizwa na Uwazi ni vipi vyuma vinaweza kuingia kwenye tumbo la binadamu, alisema:
    “Kwanza mtu asije akadhani yule mgonjwa alikula vile vyuma. Ule ni utamaduni kafanyiwa. Vyuma vinaingizwa tumboni kwa njia ya kishirikina na kukaa humo kwa muda mrefu.
    “Kinachotokea wakati vyuma vikiingia tumboni mtu anaweza kujisikia kuwashwa tumbo na kujikuna kila mara. Mara nyingi mambo hayo hufanywa na mtu ambaye ni mbaya wako, kwa kukuendea kwa waganga au kwa wachawi,” alisema mganga huyo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAAJABU 7 MAZITO ALIYETILEWA VYUMA TUMBONI MUHIMBILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top