Mashabiki
wa Bar ya Milestone Park ya jijini Arusha wakiwa wamembeba juu mchoma
nyama wa bar hiyo mara baada ya kutangazwa bingwa katika mashindano ya
Safari Lager Nyama Choma mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Nane
nane mwishoni mwa wiki
Mnadhimu
wa Jeshi la Polisi Jijini Arusha, Boniventure Mshongi (kushoto)
akimkabidhi kikombe Mchoma nyama wa Bar ya Milestone Park, Lawrence
Kimonge mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Nyama
Choma yaliyofanyika katika Uwanja wa Nanenane mwishoni mwa wiki jijini
Arusha .Katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.
Na Mwandishi Wetu.Arusha.
MILESTONE
PARK Bar jijini Ausha wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano
ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki
katika Nanenane na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja
na Kikombe.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa Royal Stop Over Bar ambayo ilizawadiwa pesa
taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Freedom Bar ambayo
ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Capital 14
Bar ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya tano ni QX Bar
ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/- Akizungumza na wakazi jiji la Arusha
walifika katika mashindano hayo, Mnadhimu wa Jeshi la Polisi jijini
Arusha, Boniventure Mshongi, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kwa kubuni mashindano hayo ambayo ni mwaka wa nane sasa
mfululizo yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi
wakazi wa Ausha kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika
baa tano ambazo zimeingia fainali katika jiji la Ausha.
Alisema
Mshongi kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa
mbalimbali za jijini Ausha ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa
kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo
tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa
jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili
aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika
baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda
hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Ausha na mwisho
aliwapongeza mabingwa watetezi ambao wametetea vyema ubingwa wao, Bar ya
Milestone Park kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma
kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo
wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa
mwaka 2015,Miliestone Park Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki
toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia
aliwashukuru wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia
nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 jijini
Arusha.
Mwisho
Edith aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema
zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016
lakini pia wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye
biashara zao.




