Balozi
wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry
Mdimu (mwenye miwani) akiongozana na wadau mbali mbali wa IMETOSHA
MOVMENT pamoja na wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakiingia
Uwanjani,ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni ya mapambano dhidi ya
mauaji ya albino yaliyobeba ujumbe wa IMETOSHA.
Sehemu
ya Wachezaji timu za Simba na Yanga wakiwa wamevalia fulana zenye
ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO,wakati wakiingia uwanjani.
Balozi
wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry
Mdimu (wa tatu kushoto) akizungumza machache juu kampeni yake ya
mapambano dhidi ya mauaji ya albino iliyobeba ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI
YA ALBILO,kabla ya kuanza kwa kipute cha Simba na Yanga uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam leo.
Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Yanga.
Beki
wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan akiwania mpira na Mshambuliaji wa timu
ya Yanga,Danny Mrwanda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Simba
imeshinda bao 1 - 0 lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na
Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Mshambuliaji
wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya
Simba,Kessy Ramadhan wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara
uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Nyanda
nambari moja wa timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwa ametulia langoni kwake
tayari kwa kuzuia shuti lililopigwa na Mshambuliaji wa Yanga,Simon
Msuva.
Wakati
mtanage ukiendelea,ghafla likatokea zogo baina ya Nahodha wa Timu ya
Yanga na Kiungo wa Simba,Abdi Banda na mambo yalikuwa hivi.
"Beki
hasififiiiii lakini hapa anastahili sifa....",Beki wa Simba,Juuko
Murshid akiruka juu kuondoa mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake,mbele
ya Washambuliaji wa Yanga.
Kipa wa Yanga,Ally Mustafa "Bartez" akiwa ameruka juu kuondoa hatari langoni kwake.
Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Simba.
Beki wa Simba,Kessy Ramadhan akimzungusha mshambuliaji wa Yanga.
Anacheza paleeeee Ivo Mapunda.
Haya nendeni kuleeeeee......
Wee kipa hili Taulo lako silitaki hapa,naliweka huku nje.
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akiachia nduki kali ambalo hata halikuzaa matunda.
Mashabiki wa Yanga wakijifariji.
Washabiki wa Simba wakiwabeza wenzao wa Yanga.
Wadau wa IMETOSHA wakiendelea kuwakilisha uwanjani.
Umati wa Washabiki wa Timu ya Simba ukiwa umefurika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam kuipa sapoti timu yao ambayo haikuwaangusha leo,baada ya kuwatandika bao 1 - 0 watani zao wa jadi Yanga,lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika kabisa.
Hatari lakongoni mwa timu ya Simbaaaaa....
Kadi
Nyekunduuuuu kwa Mchezaji wa Yanga,Haroun Niyonzimaaaaa.... baada ya
kupiga mpira ulioingia wavuni baada ya refa kupiga filimbi kuwa ni
faulo.
Niyonzima anamzonga Mwamuziii
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akizungumza na Mwamuzi juu ya Kadi aliyopewa Niyonzima.
Ukiangalia vyema utabaini kitu.
Furaha ya ushindi.