Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akipewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC maelezo ya uendelezaji wa eneo la
Usa-river lililonunuliwa na NHC kwa ajili ya kujenga Jiji la kisasa hapo
jana.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akiondoka eneo la Meru Residential arpatments alipomaliza kukagua nyumba
za makazi zilizojengwa na NHC na kuuzia wananchi hapo jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi juu ya mpango wa NHC
wa kujenga maduka makubwa ya kibiashara ili kuhudumia wananchi na wakazi
walionunua nyumba za makazi za Meru alipomtembeza Waziri huyo hapo jana
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba na kuingia ndani
kukagua nyumba hizo.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na wafanyakazi wa
NHC waliokuwa wamejipanga kumpokea Waziri Lukuvi kufungua nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
Hizi
ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani
Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba
hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha
kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana.
Mbunge
wa Longido Mhe. Lekule Laizer akilishukuru Shirika la Nyumba kwa
kuiweka Wilaya ya Longido katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa
ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika Halmashauri
mbalimbali za Wilaya hapa nchini.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akihutubia halaiki ya wananchi wa Longido (hawapo pichani)waliohudhuria
ufunguzi alioufanya wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC
Wilayani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda akilishukuru Shirika la Nyumba
kwa kujengwa nyumba Wilayani Longido eneo ambalo ni kame na lenye
changamoto kubwa ya kutekeleza ujenzi wa nyumba bora
Watendaji
wa Wizara ya Ardhi Mkoani Arusha na wananchi wakifuatilia matukio ya
ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido
jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Longido Bw. Ernest Kahindi alitoa nasaha zake wakati wa
ufunguzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ya
mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa Wilayani Longido.
Wananchi
wa Wilaya ya Longido wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali
zilizotolewa wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
na NHC Wilayani Longido
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikagua vyumba mbalimbali vya nyumba bora zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akifungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda,
Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Mchechu.
Wafanyakazi
wa NHC nao hawakuwa nyuma kumpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili mradi wa NHC
Longido kufanya ufunguzi rasmi.
Mkurugenzi
wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa
akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi alipowasili Longido kufungua rasmi nyumba za
ghrama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea kwa furaha Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC ili kufanya
ufunguzi rasmi.
Msafara
wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Vangimembe Lukuvi ukiingia eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu
zilijengwa na NHC Wilayani Longido ili kufungua rasmi nyumba hizo baada
ya kukamilika ujenzi wake.
Hizi
ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani
Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba
hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Levolosi Jijini
Arusha.Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi.Picha zote na Muungano Saguya- Longido, Arusha

