Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.
Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika viwanja vya Karume.
Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe
kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe
yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick,
amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa
mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya
uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri
taswira ya jiji la Dar es salaam.
“Tatizo
la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na
kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na
kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na
viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na
viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja ya Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Dar
es Salaam pamoja na wananchi wa Manispaa ya Ilala waliohudhuria katika
uzinduzi wa barabara ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.