Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO
machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia
kutokana na kukamilika kwa miundombinu ya mitambo ya umeme ifikapo
machi mwaka huu.
Ziara
hiyo iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na
kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la kusogeza miundombinu ya
umeme karibu na watumiaji wa umeme.
Simbachawene
amesema kuwa kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa
uhakika inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n
amatatizo ya umeme.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba amesema kuwa matatizo
mbalimbali ya ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa
kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme
ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na wandishi wa
habari katika Ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa miradi ya umeme jijini Dar
es Salaam leo.
Waziri
wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo na
Manirabona Emmanuel meneja wa Project wa TANESCO kuhusiana na
uboreshaji wa mitambo ya Umeme ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa project wa Tanesco Manirabona Emmanuel akimwonyesha Waziri wa
Nishati na Madini,George Simbachawene jinsi mitambo ya Umeme itakavyo
jengwa katika Mitambo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
Mitambo ya umeme ya Mbagala jijini Dar es Salaam. Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.