BALOZI WA FINLAND NCHINI TANZANIA ,ANTILA SINIKKA AZINDUA KITUO CHA MSAADA KWA WAHANGA WA UKATILI.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akiwa katika picha ya pamoja na watoa ushauri.
Balozi wa
Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara baada ya
kufungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo
hicho.
Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza kwa niaba ya wadau wa Kwieco wakati wa sherehe hizo.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akikata utepe kuashiria kuazna kutumika kwa majengo hayo.
Mjumbe wa
bodi ya wakurugenzi wa KWIECO,Jaji Aishiel Sumari akitoa neno la
shukrani mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi ,Balozi wa Finland Tanzania
Mh. Antila Sinikka.
Balozi wa
Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia,mradi unaofadhiliwa
na Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje chini ya shirika
la UKUMBI.
Katibu
tawala wa mkoa a Kilimanjaro ,Martha Ufunguo akitoa salama za mkoa kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Mkurugenzi
wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu
mkoani Kilimanjaro(KWIECO) Elizabeth Minde akitoa hotuba yake wakati wa
uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Katika
kituo hicho wahanga watapatiwa malazi ya muda na huduma zingine za
kijamii km matibabu, chakula, msaada wa kisheria, mafunzo ya
ujasiriamali n.k.
Mjumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi ya KWIECO ,Clement Kwayu akitoa neno la ukaribisho
kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Loe Rose Mbise wakai wa sherehe ya
uzinduzi wa kituo hicho.
Balozi wa
Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara wakati
akitembelea majengo ya kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa
kijinsia ambayo yamejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia
wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo chini ya shirika la UKUMBI.
Balozi wa
Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka alikabidhi kitabu cha "Politics of
Gender "kwa mkurugenzi wa Kwieco ,Elizabeth Minde.
Watoa
ushauri wa shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za
binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO)wakiimba wakati wa ufunguzi wa kituo
hicho.
Mkurugenzi
wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu
mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Mh.
Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa
wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Maeneo mbalimbali ya kituo hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.