https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Kafulila: JK kavunja uchumi aliouweka Mkapa



    Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
    Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa

    DAVID  Kafulila, mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR – Mageuzi) amesema, “Rais Jakaya Kikwete, amevunja misingi ya uchumi iliyoasisiwa na mtangulizi wake, Rais Benjamini Mkapa.” 
    Amesema, “Mkapa amepokea nchi mwaka 1995, huku ukuaji wa uchumi ukiwa asilimia 4.2. Alipoondoka madarakani uchumi ulikuwa asilimia 6.7. Leo Rais Kikwete ameushusha hadi asilimia 6.4.” Anaandika Pendo Omary … (endelea).
    Akichangia Bajeti ya serikali jana jioni na baadae katika mahojiano maalum na MwanaHALISI Online, mbunge huyo machachari anasema, kilichopaswa kufanywa na Rais Kikwete ni kulinda mafanikio yaliyoachwa na Mkapa.
    Amesema, mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa asilimia 21 lakini mwaka 2005 mfumko huo ulishuka mpaka asilimia 4.

    Lakini anasema, kwa sasa mfumko wa bei, umefikia asilimia 5.3.
    Kwa upande wa riba ya benki, Kafulila amesema, Mkapa alipokea serikali riba ya benki ikiwa asilimia 30 hadi 26 mwaka 1995. Mwaka 2005 riba ya  benki ilishuka hadi asilimia 14. 
    Akiongea kwa uchungu, Kafulila amesema, chini ya utawala wa Kikwete, riba ya benki imepanda hadi asilimia 18.
    Akizungumzia ukuaji wa uchumi wa sekta binafisi, Kafulila amesema, wakati Mkapa anaingia madarakani mwaka 1995, akiba ya fedha za kigeni zilikuwa za miezi miwili; hadi mwaka 2005, akiba hiyo ilifikia ya miezi nane.
     “Mkapa kapewa nchi ikiwa haikopesheki mwaka 1995. Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa Sh 10 trioni. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, deni limefika Sh. 35 trioni. Ziada ya Sh. 25 trioni na kilichofanywa na deni hakionekani.
    “Kupitia deni hili ilipaswa tuoneshwe reli ya kati imejegwa na bandari zote za Mtwara, Dar es Salaam, Kigoma, Mwanza na Tanga. Ni  bahati mbaya, sehemu kubwa ya deni hili, limetokana na matumizi ya kawaida,” ameeleza Kafulila kwa sauti ya uonyonge.
    Kuhusu mapato ya taifa, Kafulila amesema, Mkapa aliacha nchi ikiwa inakusanya mapato ya ndani zaidi ya asilimia 14 ya pato la taifa mwaka 2005. Kwa sasa, kodi inayokusanywa ni asilimia 12 ya pato la taifa.
    Amesema serikali inaongeza kodi ya mafuta kwa sababu ya kupeleka umeme vijijini, lakini serikali imeshidwa kutumia vyanzo vingi kujipatia mapato ikiwemo;
    Mosi, tangu mwaka 2007 serikali igoma kununua mtambo wa kurekodi matumizi ya simu ili iwe na uhakika wa mapato ya kampuni hizi. Matokeo yake kampuni hizo zinavuna fedha nyingi lakini serikali inapata kodi kidogo.
    “sheria ya mawasiliono ya mwaka 2009 ilotaka. Ndani ya miaka mitatu kampuni zote ziwe zimeorodhesha hisa zao soko la mtaji la DSE ili mapato na matumizi yafahamike na umma uweze kuwa sehemu ya ya wamiliki. Serikali imeshindwa kutengeneza kanuni za kutekeleza sheria  hiyo mpaka leo,” amesema Kafulila.
    Pili, kodi za uvuvi bahari kuu bado tatizo. Nchi ya Namibia ukanda wake wa bahari kuu ni karibu sawa na Tanzania. Wao ni 1500 Km, Tanzania ni 1424 Km. Wakati uvuvi nchini Namibia ni chanzo cha pili cha pato la taifa. Tanzania inaacha meli zinavua bila kulipa kodi.
    Tatu, mgodi wa Mwadui  uliopo Mkoa wa Shinyanga unaendesha shuguli zake nchini tangu  tangu mwaka 1944. Na tangu uhuru hawalipi kodi kwa kutangaza hasara laki hawaendi kwao.
    “Hali ya nchi ni mbaya. Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye misitu mikubwa ya mbao afrika lakini tuna upungufu wa madawati 1,170,000. hii ni kwa mujibu wa taarifa ya HAKI ELIMU. Kama kila dawati wanakaa wanafunzi3 maana yake tuna zaidi ya watoto 3milioni wanakaa chini,” Kafulila amefafanua.
    Aidha, ameeleza Tanzania inaongoza kwa kuwatoza kodi kubwa wafanyakazi kuliko nchi zote afrika mashariki. Inatoza wastani wa asilimia18 . Wengine walichanganya na kima cha chini cha kodi ya asilimia 11.
    Wastani wa kodi nchini ni asilimia 18. Kwani kuna wafanyakazi wanatozwa kodi asilimia30. Nchi ya rwanda wastani wa kodi ya mshahara ni asilimia 5.6, kenya asilimia 6.8, Burundi asilimia 10.3 na Uganda asilimia 11.
    “Hii ni dunia ya soko huria. Ni dunia ya ushindani. Tunahitaji rais ambae atatengeneza watanzania weledi na wenye juhudi ili hata gesi na madini visipokuwepo wataishi hata nchi ikigeuka jangwa,” Kafulila ameongeza.
    Mbali na changamoto hizo ripoti ya Shirika la Msaada wa Watu wa Marekani (USAID) ya Mei mwaka huu inaonesha asilimia 34 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa umasikini.

    credit: http://mwanahalisionline.com
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Kafulila: JK kavunja uchumi aliouweka Mkapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top