Lowassa akiendelea kuzungumza katika mkutano huo.
Edward Lowasa akizungumza jambo katika mkutano wa leo Mkwajuni, Kinondoni, Dar.Mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi, Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza jambo katika mkutano huo.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Mke wa Lowassa, Regina akisalimia wananchi waliohudhuria(hawapo pichani).
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wake kwa kishindo katika mkutano uliofanyika katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni leo.
Lowassa amepata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar, ambapo amepata zaidi ya wadhamini 95,251 huku akisema ni zaidi ya mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo Lowassa amesema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa na maneno ya watu yanayovumishwa ya kuwa anawapatia fedha ili wafike mkutano wake na makundi ya watu kuwa wanaosema kuwa hafai kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wapuuzwe.
Aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi ndani zaidi ya miezi sita tayari matokeo yatakuwa yameonekana.
“Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua epukane nayo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment