Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki
(katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali
Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea
wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana
mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa
Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri
wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja
vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio
,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa
hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili
wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara
katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima
za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri
wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja
vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media
wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati
wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Safari ya kuelekea Kagera kwaajili ya maziko ya Mwili wa Mhariri wa Mawio
,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri
wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio
na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya
habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari .
Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara
ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi
kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa
wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbow.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi
amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia
misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri
kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema
Mengi.