Mlio kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hongereni kwani ni moja ya nguzo kuu ya Uislamu.
Sehemu kubwa ya jamii yetu kuna mambo yamekuwa yakifanyika na kuonekana kana kwamba ni mambo ya kawaida lakini ukweli si huo.
Wapenzi kuchepuka imekuwa kama sehemu ya maisha yao ya kila siku hasa kwa wanandoa, kama vile kula na kunywa bila kujali kuvimbiwa.
Baadhi ya wapenzi, bila kujua kuwa michepuko siyo dili na michepuko mingine ni nuksi katika maisha yao wamejikuta nao wakijikwaa kwenye dhambi hiyo.
Kuna misemo mingi ya kejeli, dharau, majigambo na mingineyo ambayo imekuwa ikizungumzwa na jinsi ya kiume kwa kuisema jinsi ya kike. Eti utasikia ‘yule mwanamke ni nuksi bwana sisi tulikwambia tunamfahamu, ukajifanya unajua kupenda haya sasa umejionea mwenyewe’.
Na sehemu kubwa ya jamii yetu inaamini kuwa mwanamke pekee ndiye mwenye majanga. Baadhi wanaamini tatizo la kutokupata mtoto huwa ni la mwanamke tu, pasipo kufahamu kwamba hata wanaume nao wapo baadhi wenye nuksi.
Naandika makala haya ili tujifunze. Ni kweli kabisa kuna michepuko mingine ni balaa.
Unaweza ukajifanya mjanja na msiri kwa kuchepuka nje ya ndoa yako au uhusiano wako, ikawa ni shida na kila aina ya mikosi ikawa inakuandama.
Kuna baadhi ya michepuko imeshindwa kuolewa au kuoa kwa sababu tu ya gundu iliyonayo. Kila mpenzi aliye naye anaandamwa na majanga mara kwa mara.
Unaweza ukawa na mrembo mkali au jamaa mzuri lakini ukiangalia tangu umekuwa naye katika uhusiano, dili zako haziendi sawa, fedha hakuna, zikipatikana hazikai, kazini kunawaka moto, ulipopanga baba au mama mwenye nyumba anazingua ilimradi utata mtupu katika maisha yako.
Na hii inawakuta sana wanandoa. Unaweza ukajidanganya kuchepuka, kumbe umechepukia kwa mtu mwenye tatizo au kimeo ambacho kitaharibu kabisa ndoa yako na mfumo mzima wa maisha yako.
Mfano kazini ukafukuzwa au kushushwa cheo, watoto nao shuleni wakafukuzwa kisa, kukosa ada, kodi ya pango inasumbua, mara gari la mkopo nalo limeteketea kwa moto na mbaya zaidi hata nusu ya mkopo uliokopa hujarejesha.
Itaendelea wiki ijayo, usikose!
0 comments:
Post a Comment