Mwanamke raia wa Tanzania aitwae Chambo Fatma Basil, amekamatwa katika uwanja wa ndege wenye harakati nyingi wa Mumbai akiwa na kilo 74 za dawa za kulevya aina ya methaqualone.
Maafisa wa Uhamiaji na wa Usalama walimkamata mwanamke huyo, jumatano akiwa na paspoti ya Tanzania akijianda kuja Dar es Salaam kupitia Doha, baada ya kupatiwa taarifa za kishushushu.
Baada ya kufanyiwa upekuzi ilibainika kwenye mabegi yake matatu kulikuwa na pakiti zenye unga mweupe na uchunguzi zaidi ulibaini unga huo ni dawa za kulevya aina ya methaqualone ama Mandrax, ambayo ni kilevi cha bei rahisi kuliko cocaine.