Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
HAKUWAMO hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba wa Yanga wakati timu hiyo ya Jangwani ilipofungwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia katika mechi yao ya kwanza ya Kundi A la Kombe la Kagame Jumamosi iliyopita.

Alianzia benchi katika mecjhi ya pili ya kundi hilo Yanga iliposhinda 3-0 dhidi ya vibonde wa kundi, timu ya Telecom ya Djibouti, lakini akaingizwa dakika ya kwanza kati ya tatu za nyongeza na aligusa mpira mara moja kisha refa akamaliza pambano.
Leo tena ameingizwa dakika ya kwanza kati ya tatu za nyongeza katika mechi ambayo Yanga imeshinda 2-0 dhidi ya KMKM kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa ikiwa ni mechi ya pili kwa mabingwa hao mara 25 wa Tanzania Bara kushinda kwenye Kombe la Kagame mwaka huu.
Katika mechi ya leo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho hakuugusa mpira hata mara moja kabla ya kipenga cha mwisho cha refa wa kati Souleiman Djama kutoka Djibouti kupulizwa.
Kuna nini kwa Coutinho na benchi a ufundi la Yanga? Kauli ya kocha mkuu wa Yanga, Mdachi Hans van dedr Pluijm, inafuata juu ya suala hili.
0 comments:
Post a Comment