Cristiano Ronaldo ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania, mara nyingi akiwa anakula good times zake utaona jamaa yuko na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior na huwa anamuwekea ulinzi wa kutosha kila anapokatisha.
Cristiano Ronaldo Junior alizaliwa June 17 2010 San Diego Marekani wakati ambao Ronaldo alikuwa Afrika ya Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, Ronaldo alitangaza 3 July 2010 kuhusu kupata mtoto kupitia account yake ya Twitter na Facebook siku chache baada ya Ureno kutolewa na Hispania katika michuano ya Kombe la Dunia.
Baada ya Ronaldo kutangaza taarifa hizo za kuwa baba wengi wamekuwa wakijiuliza na kutaka kumjua mama wa mtoto huyo licha ya Ronaldo
kutotaka kumuweka wazi baada ya maelezo aliyoandika katika account zake
Mitandaoni kwamba hiyo kitu inahusu maisha yake binafsi na haitaji
kuweka wazi.
“Nikiwa na
furaha tele na hisia za kuwataarifu kwamba hivi karibuni nimekuwa baba
wa mtoto wa kiume. Kama nilivyokubaliana na mama wa mtoto kuwa jambo
hili kuwa siri. Mwanangu atakuwa chini ya uangalizi wangu. Naomba kila
mtu aheshimu haki ya kuwa na usiri angalau kwa masuala binafsi kama
haya”>>>Ronaldo
Licha ya kuwa mama wa mtoto hajulikani ila kumekuwa kuna taarifa za kichunguzi amabazo zinasema miezi kadhaa baada ya Cristiano Ronaldo Jr kuzaliwa mama yake alifariki lakini taarifa nyingine zinasema Cristiano Ronaldo Jr alizaliwa na kwa njia za kitechnolojia (Surrogate Mother) ambapo mwanamke wa kimarekani alilipwa na Ronaldo pound milioni 10 ambayo sawa na bilioni 32 za kitanzania ili abebe ujauzito kiteknolojia zaidi.
Baada ya malipo kufanyika Ronaldo na mama wa mtoto wake wamekubaliana kisheria kuwa asije akajitokeza hadharani na kusema yeye ni mama wa mtoto wa Ronaldo.
0 comments:
Post a Comment