Mkongwe na nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard amemjia juu mchezaji mwenzake wa zamani Raheem Sterling ambaye amezua ‘sekeseke’ la kutaka kuihama klabu hiyo hadi kufikia kutaka kugoma kusafiri pamoja na timu kwenda kwenye ziara kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao (pre-season tour) ili kushinikiza klabu hiyo imuache aondoke.
Gerrard amesema, Sterling hana haja ya kuonesha tabia anayoionesha kwa sasa kwenye klabu. Ameshauri kuwa, ni vyema kinda huyo akakaa na kuzungumza na klabu kuliko kufanya hayo anayoyafanya kuanzia wiki hii.
“Kuna mamilioni ya mashabiki wa Liverpool kote duniani ambao wanatamani kumuona Raheem akiwa ndani ya uzi wa Liverpool. Kwahiyo sioni kama ni jambo la kiungwana kwa Raheem kuonesha tabia hii”, amesema Gerrard.
Manuel Pellegrin hana haraka ya kuamua ni ofa ya kiasi gani itakuwa ya mwisho kuipelekea Liverpool akiamini uhusiano mbovu unaoendelea kati ya Liverpool na Sterling unaweza ukapelekea klabu hiyo kupunguza msimamo wao wa kutaka kitita cha pauni milioni 50 ili wamuachie nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment