Club ya Simba imetoa tamko kupitia ukurasa wao wa facebook na kuweka wazi kila kitu pamoja na kumtakia heri Emmanuel Okwi huko aendapo. Hii ni statement ya Simba.
“Kwa kutambua umuhimu wa kuwapa taarifa za uhakika wanachama na wapenzi wa Simba, Uongozi wa Simba unapenda kuwataarifu rasmi kuwa mchezaji Emmanuel Okwi amefanikiwa vipimo na kusajiliwa kwa dola za kimarekani 110,000 kwenye klabu ya ya Sonderjyske nchini Denmark.
Ikumbukwe kwamba Emmanuel Okwi alikuwa amebakiza miezi 9 kumaliza mkataba wake uliotarajiwa kuisha April 2016. Mkataba huu ulikuwa na kipengele kinachoeleza kuwa ikiwa mchezaji akipata timu basi Uongozi utamruhusu. Jambo muhimu la kuzingatia ni kuwa katika sharia za uhamisho na mikataba ya wachezaji ikiwa mkataba unaisha basi mchezaji anakuwa huru kuhama bila timu kupata malipo yeyote.
Pamoja na uhamisho huu, Uongozi wa Simba ungependa kujulisha wapenzi wa Simba kuwa hadi sasa bado haijatoa kibali cha uamisho yaani International Transfer ambacho huwa wanapewa wachezaji wa kimataifa hadi malipo yatakapofanyika.
Uongozi wa Simba unatarajia kuzitumia fedha hizi kwa ajili ya usajili wa wachezaji wa kimataifa ili kuziba pengo la Mchezaji Emmanuel Okwi.
Simba mara zote imejitahidi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wachezaji wake wenye vipaji kuweza kuboresha vipaji vyao na maisha kwa kuwapa fursa ya kufanya majaribio au kuhamia timu za nje.
Simba mara zote imejitahidi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wachezaji wake wenye vipaji kuweza kuboresha vipaji vyao na maisha kwa kuwapa fursa ya kufanya majaribio au kuhamia timu za nje.
Tunaamini kwa dhati Simba itaziba pengo la Emmanuel Okwi na kujenga timu bora.
Okwi alizaliwa Desemba 25, 1992 Kampala Uganda anachezea timu ya Taifa ya Uganda kama mshambuliaji wenye jezi namba 10.
Uongozi, wanachama wa Simba na Simbasports.co.tz wanamtakia kila la kheri katika klabu ya mpya. #miminimemba ”
Uongozi, wanachama wa Simba na Simbasports.co.tz wanamtakia kila la kheri katika klabu ya mpya. #miminimemba ”
0 comments:
Post a Comment