Hivi unazani JK Nyerere angekuwa mchezaji tungemfananisha na nani?
Anyway achilia kuhusu mbali Mwalimu, mfano Diamond platnum nae
angekuwa mwanasoka tungekuwa tunaongea nini sasa hivi? au wale akina
Flaviana Matata je, wangekuwa wanariadha kama wale wadada wa ki Kenya
au Ethiopia tungekuwa na medali ngapi? nazani kuna haja ya kumuomba
Mungu tupate wakina Samata 40, akina Diamond wa soka 10 tu na Nyerere
wa soka 1 tu, inawezekana na sisi siku moja tukawa na wachezaji walau
wawili kwenye list ya wachezaji bora watatu wanaowania tuzo ya
mchezaji bora wa UEFA wa msimu.. inawezekana ninaota mchana kweupe…!
Tunapozungumzia wachezaji hodari duniani, bila ajizi lazima utamulikaAnyway achilia kuhusu mbali Mwalimu, mfano Diamond platnum nae
angekuwa mwanasoka tungekuwa tunaongea nini sasa hivi? au wale akina
Flaviana Matata je, wangekuwa wanariadha kama wale wadada wa ki Kenya
au Ethiopia tungekuwa na medali ngapi? nazani kuna haja ya kumuomba
Mungu tupate wakina Samata 40, akina Diamond wa soka 10 tu na Nyerere
wa soka 1 tu, inawezekana na sisi siku moja tukawa na wachezaji walau
wawili kwenye list ya wachezaji bora watatu wanaowania tuzo ya
mchezaji bora wa UEFA wa msimu.. inawezekana ninaota mchana kweupe…!
wale waocheza Ulaya hasa zile ligi maarufu, pale Ulaya kuna watu wana
vipaji bwana…! yani kuna jamaa mmoja kasafiri karibu 10671 km kutoka
Argentina hadi pale Spain, japokuwa wapo wengi, ila huyu ni miongoni
mwa wachezaji bora kabisa Ulaya tangu 2008 hadi sasa… kwa watu wenye
imani duni lazima watahisi kuwa hivi vipaji sio vya kawaida.!
Nimeshawasikia watu wengi wakiwahusisha wachezaji wengi wanaocheza
Ulaya na kile chama maarufu kinachomuabudu Shetani, ila kwa sisi
wadadisi wa mambo tunaamini katika mazoezi na juhudi tuu..
Nikiwa naangalia “Highlight” najikuta napiga kelele za mguno wa
kushangaa.!! hii ni mara baada ya kumuona kijana mfupi ambaye sio
muongeaji na mara nyingi hapendi kucheka ovyo, kijana huyu ukiangalia
cheza yake utahisi ni mzimu maana sekunde yupo hapa, baada ya sekunde
5 tena yupo umbali mrefu sana tena kashapiga vyenga watu 6…!! naomba
tuwe pamoja kutazama mafanikio ya huyu “Njiti” msimu uliopita na kuona
je anastahili kuingia “Top 3″ ya kuwania tuzo ya mchezaji bora
anaecheza Ulaya..? Tafadhali naomba twende pamoja hadi mwisho wa
makala hii fupi ndani ukurasa huu unaoongoza kwa michezo hapa
Tanzania..
Mnamo tar 12 August, Ulaya na Dunia itakuwa na shauku ya kuona na
kusikia ni nani hasa anastahili kuingia “Top 3″ kati ya wale
wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa UEFA, kuna jamaa mmoja ambaye “by
any means” lazima naye atakuwepo kwenye list ya wachezaji watatu.!
tena huyu pia ana nafasi kubwa ya kutwaa, juzi niliandika kidogo
kuhusu Neymar kwamba inawezekana akaingia kwenye list.! lakini huyu
kwa mambo aliyoyafanya ni lazma atakuwepo kwenye list ya wale watatu
na kuna uwezekano mkubwa tena zaidi ya 53% akachukua tuzo hii, naomba
tujadili mafanikio yake japo kwa ufupi hapa chini..
Japokuwa yeye ni mshambuliaji muongo muongo aliyempisha Suarez
kusimama kama mshambuliaji rasmi pale Camp Nou, “mchawi mweupe” Lionel
Messi ametupia magoli 58 katika mechi 56 pale Ulaya, hapa namaanisha
akiwa na klabu yake, kwa magoli haya tuu ni kigezo tosha cha kuingia
top 3.! ila sio kigezo cha kuchukua tuzo kwani kama kuchukua tuzo ni
magoli yupo fundi mwingine ambaye hata tukiskia kafunga 10 kwenye
mechi moja hatushangai, yeye yupo pale jiji la Madrid. Msimu uliopita
Messi alifunga magoli 58 kati ya yale 122 yaliyofungwa na utatu
utakatifu, ukipiga hesabu hapo amefunga 48% ya magoli yote….
Kikubwa zaidi ambacho kinampa nafasi ya kuchukua tuzo hii, kwanza ni
kuiwezesha timu yake kutwaa ubingwa wa La liga ambapo alifunga magoli
43 na kuwa mfungaji bora wa pili nyuma ya Cr7, magoli kwenye La liga
sio tija bali zile “assist” 18 ambazo zimemfanya kuwa “highest
assister” kwenye soka unapotoa pasi ya goli basi na wewe umehusika
kufunga kwa kiwango kikubwa, hapa ndo Mchawi mweupe kawazidi wenzake,
kumbuka pia “assist” yake ndo ilimpa Suarez goli la kwanza pale Fc
Barcelona. kabla ya msimu uliopita hapa alikuwa na magoli 28 kwenye La
liga na 15 “assist” lakini kwenye michuano yote..!
Kama kawaida yake Messi pia ameiwezesha kwa kiwango kikubwa timu yake
kutwaa kombe la Mfalme, kumbuka kiwango chake kwenye kombe hili tangu
hatua za awali hadi fainali..! bila shaka Messi alikuwa na msimu mzuri
sana ndio maana katoa mchango mkubwa kwa timu yake kutwaa “Trebble”,
kumbuka hapa pia alifunga magoli 5 katika mechi 6 huku akitoa “assist”
4, Mungu akupe nini Messi..!!! nazani unamkumbuka “man of the match”
kwenye mechi ya fainali ya kombe hili, pia yale magoli 7 Neymar
aliyofunga kwenye kombe hili kwa kiwango kikubwa yalichagizwa na
Mchawi mweupe, naamini hiki ni kigezo tosha kutwaa tuzo hii…
Kwenye UEFA, hapa ndo Messi alifanya makubwa, nazani moja kwa moja
unavuta picha kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Bayern, achilia
mbali hiyo, vipi magoli 10 aliyofunga katika mechi 13 za UEFA huku
akitoa “assist” 6 na hatimaye kuwa “Top assister” tena kwenye kila
kombe aliloshiriki msimu huu. Hapa pia kaiwezesha Fc Barcelona kutwaa
kombe hili kubwa kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya. Kumbuka hata magoli
10 ya Neymar yamechangiwa na Messi kwa kiwango kikubwa. Bila shaka
hata kuvaa medali ya UEFA msimu uliopita kunampa Messi nafasi ya
kutwaa tuzo hii tofauti na wapinzani wake.
Wapenzi wengi wa soka hasa wale watazamaji hupenda sana kumuona
mchezaji akipiga vyenga wachezaji zaidi ya wawili tena kwa chenga za
mauzi, japokuwa Messi hajafikia vyenga vya Gaucho ila unapozungumzia
wachezaji wanao “dribble” sana Duniani tena kwa vyenga vya mauzi
huwezi acha kumtaja mchawi mweupe, hadi sasa anakabana koo na akina
Hazard ila yeye anaonekana bora kabisa katika eneo hili, bila shaka
unakumbuka mechi dhidi ya Billbao, Man city, Bayern, Juve, Atlettco
n.k …! Hizi ni chache sana ila hapa ndo sehemu ambayo atawapiku
wapinzani wake na hatimaye kutwaa tuzo hii yenye heshima kubwa Ulaya.
Tukisema tumzungumzie kwa mapana Messi hatutamaliza leo, naamini
Shaffih na wachambuzi wengine wa michezo duniani wameshamjadili sana
huyu jamaa, ila kwa leo ngoja nitie nanga hapo ila kama kawaida jicho
langu la tatu linamuona Messi 27 August akitajwa mchezaji bora wa UEFA
ila kabla ya hapo namuona kweny namuona Messi akiiwezesha Barca tena
kutwaa kombe zaidi ya moja msimu ujao, mimi na wewe tuseme “in shaa
allah” tushuhudie mengi msimu ujao kutoka kwake..
0 comments:
Post a Comment