Ni ngumu sana kwa mchezaji yoyote duniani kufikia ndoto nyingi na kubwa kama Casillas. Japokua kuna ndoyo moja ambayo bado haijakamilika na haitakamilika tena. Hivi sasa Casillas atahamia umbali ambao itabidi atumie dakika 45 kwa safari ya ndege kurudi kwao kwenye jiji la Madrid.
Kwenye moja ya interview ya Iker Casillas ambayo ilifanyika October mwaka jana inathibitisha kwamba Iker alikua na ndoto maishani mwake ya kucheza soka ndani ya Madrid na kumaliza hapo hapo. Iker alisema hivi “Real Madrid ni nyumbani kwetu, Sikuwai kuwa na majirani sana au hata vikundi vya shuleni. Nilikua na miaka 8 nilivyoanza kucheza mashindano na wakati nina miaka 9 walinisaini. Nikuja hapa kwa hatua na napaona hapa ni nyumbani kwetu. Siku zote nimekua sehemu ya Madrid na nimekua kama mchezaji na binadamu wa kawaida kwa malezi ya hapa hapa. Mimi nimekua hapa na kuwa na kumbukumbu zote hapahapa”
Iker alisema kwamba sio rahisi na vigumu kumuona yeye yupo ndani ya jezi ya Club nyingine, “Ni vigumu kufikiria mimi kwenye club nyingine. Nistafu mpira nikiwa hapahapa. Japokua nigependa kujaribu ligi nyingine ili niweze ku-appreciate Madrid zaidi kwani huko hakutakua kama hapa.”
Ndoto pekee ya Iker na sio rahisi kutimia ni swala la yeye kumaliza soka ndani ya Madrid.
0 comments:
Post a Comment