Kampuni ya Microsoft (MST Tech 30) ni miongoni mwa kampuni kubwa za teknolojia duniani, wakiwa ni watengenezaji wakubwa wa bidhaa za kompyuta na simu duniani.
Kampuni ya Microsoft ilikuwa na wafanyakazi 118,600 mpaka mwezi March 30 2015, kati yao wafanyakazi 60,000 walikuwa ndani ya Marekani… Mwaka 2014 kampuni hiyo iliwasimamisha kazi watu 18,000.. wengi walishangazwa na uamuzi huo.
Story kubwa kuhusu wao leo inahusu Kampuni hiyo kutangaza tena kuwasimamisha kazi wafanyakazi 7,800 na hawatatoka Marekani tu bali kwenye matawi yao yaliyoko sehemu mbalimbali Duniani.
Maamuzi haya hayajapokelewa vizuri na watu wengi, kati ya watakaopoteza ajira zao safari hii watu 2,300 wanatokea Finland.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Satya Nadella amesema sababu ya wao kupunguza tena idadi ya wafanyakazi wao duniani imesababishwa na mfumo mpya wa uendeshaji wa kampuni na mfumo mpya wa ufanyaji biashara wa kampuni hiyo.
0 comments:
Post a Comment