https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Presha juu CCM


    Dodoma/Z’bar. Wakati vikao vya juu vya CCM vya kuchuja wagombea urais vikianza leo, hofu na wasiwasi umezidi kutanda miongoni mwa wagombea, viongozi na wanachama wa chama hicho kuhusu namna ya kuikabili minyukano baina ya wagombea hao na kibarua cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
    Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa miongoni mwa mambo yanayoleta hofu na kusababisha presha kuongezeka kila kukicha ni woga wa kufanya makosa katika uteuzi wa ndani, hali inayoweza kukigharimu chama hapo baadaye hasa kutokana na kuongezeka nguvu ya upinzani.
    Kutokana na hali hiyo kumekuwa na shinikizo kutoka katika makundi mbalimbali chama hicho kuwa makini kumteua mgombea anayekubalika, msafi na mwenye kuchagulika ambaye atatoa ushindani kwa wagombea wa upinzani, hasa Ukawa.
    Vilevile, kumekuwapo na wasiwasi wa baadhi ya wagombea kutishia kukihama chama hicho endapo majina yao yatakatwa, jambo ambalo pia linakiweka njia panda.
    Nape: Hakuna shinikizo
    Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amejibu hoja hizo akisema chama hicho hakitafanya uamuzi kwa kushinikizwa na watu, bali kitafuata taratibu na kanuni.
    “Tunazo taratibu, tunazo kanuni zetu. Nataka kuamini kuwa kila mtu aliyegombea anajua kuna kushinda na kuna kushindwa na kuna kuteuliwa na kutokuteuliwa,” alisema jana alipozungumza na waandishi wa habari.
    Alisema hataki kuamini kuwa kuna mgombea kati ya 38 walioomba nafasi hiyo ambaye anaamini anaingia kushinda tu.
    “Usipokuwa wewe anakuwa mwingine... Asiyekubali kushindwa basi atakuwa si mshindani. Usisahau hizo ni presha za wapambe hazitupi tabu. Tunachojua walioshindwa watapeana mkono na aliyeshinda na chama kitabaki kuwa kimoja,” alisema Nape.
    Alisema wananchi waamini chama kitatenda haki, taratibu zitafuatwa na kuwapa mgombea bora.
    “Haya ni maneno ya presha za barabarani ninachoamini mwisho wa siku hakuna fujo, hakuna vurugu, vyombo vimejipanga vizuri hakuna vurugu na wapambe kusindikizana ni jambo la kawaida,” alisema na kuongeza kuwa anafahamu kuwa wapo watakaohuzunika kutokana na majina ya watu wao kukatwa lakini hakuna jinsi kwa sababu kanuni za CCM zinasema Kamati Kuu (CC) itapendekeza majina matano kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
    Pia kanuni hizo zinasema NEC itapendekeza majina matatu kwa mkutano mkuu ambao utachagua mmo
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Presha juu CCM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top