Watu wanne wamefariki dunia leo na wengine 21 kujeruhiwa kufuatia basi aina ya Isuzu kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikienda bara katika kilomita 276/0 kati ya stesheni za Kimamba na Kilosa Mkoani Morogoro wilayani Kilosa majira ya saa 11:25 asubuhi ya leo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elia Mshana amesema basi hilo lenye namba za usajili T 837 CTM Isuzu Coaster linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa Kilosa.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye ajali hiyo ilitokea leo July 1 huko wilaya ya Kilosa Morogoro
0 comments:
Post a Comment