WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zinatarajiwa kuanza kesho kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Ngoyai Lowassa na Rais Jakaya Kikwete wapo katika vita kali ya kisiasa.
Vita hiyo ambayo kwa sasa ipo dhahiri imetokana uhusiano mbaya kati yao tangu alipojiuzulu kwa uwaziri mkuu kwa kashfa ya Richmond na sasa uhusiano wao umezidi kuwa mbaya zaidi tangu alipoenguliwa na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kuwania urais kupitia chama hicho baada ya kutyokidhi vigezo ikiwamo kukiuka kanuni za cha chama, ufisadi na kutokuwa mwadilifu katika kuitumikia nchi.
Baada ya tukio hilo, Lowassa aliamua kukimbilia chama cha upinzani (Chadema), na kutumia muda mwingi katika majukwaa ya kisiasa kukikashfu chama alimokulia (CCM), kwamba kimepoteza mwelekeo na kuongeza kwamba sera zake haziwezi kuliletea taifa maendeleo jambo ambalo limekuwa likimchukiza rais Kikwete ambaye naye amejitokeza adharani kuwa viongozi akimlenga Lowassa kuwa kiongozi mlarushwa hafai kuingoza nchiWakati Lowassa amekuwa akitumia gharama kubwa kujinadi kupitia Ukawa,Rais Kikwete amezifananisha harakati hizo kama moto wa mabua ambao huwaka kwa kasi na kuzimika baada ya muda mfupi, na kuongeza kwamba Magufuli atamshinda kimkakati kwa kunadi sera bora zilizomo katika Ilani ya uchaguzi ya CCM na si matumizi makubwa ya fedha kama anavyofanya Lowassa kununua uongozi kwa nguvu.
Rais JK wakati akimnadi Lowassa enzi hizo akiwa CCM.
Uhasama wao umekuwa ukiongezeka siku hadi siku, baada ya Lowassa kujiona kama ana nguvu ya kisiasa hivyo kusema chochote atakacho ikiwamo kumkasfu Rais Kikwete kuwa ameharibu uchumi, jambo ambalo linamhusu yeye moja kwa moja kwani aliitumikia serikali ya CCM kwa kipindi kirefu mpaka hapo alipolazimishwa kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa isiyovumilika. (Richmond).
Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema kuwa wakati wa kampeni Kamati ya ushindi ya mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli ikiongozwa na Rais Kikwete ina mikakati mizito ya kumsambaratisha Lowassa licha ya kwamba amekuwa akijigamba kuwa Oktoba 25 atatangaziwa ushindi wa kuingia ikulu asubuhi ‘kweupe’, jambo ambalo CCM inalichulia kama kelele zap aka zisivyoweza kumzuia mwenyenyumba kupata usingizi.
Lowassa naye anajinasibu kuwa anaiamini kamati yake ya ushindi kuwa itamwezesha kwenda Ikulu, jambo ambalo CCM imekuwa ikilipuuza.


0 comments:
Post a Comment