Huyo ni Mh Harrison Mwakyembe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule
ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond iliyomwondoa madarakani
aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya awamu ya tatu ambaye kwa
sasa ni mgombea wa kiti cha urais kupitia umoja wa vyama vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kwa tiketi ya Chadema Mh Edward
Lowassa wakati akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Kyela mkoani Mbeya
kuhusiana na sakata hilo kwamba Mh Lowassa hakusingiziwa na
kutahadharisha kuwa kesi ya jinai haina ukomo.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Mh Mwigulu Lameck
Nchemba amewatahadharisha watanzania kutopeleka viongozi aliowaita
wasaka dili ikulu kwa kuwa majuto ni mjukuu.
Katika mojawapo ya mikutano ya hadhara iliyofanyika mkoani Mbeya
hii leo katika wilaya ya Rungwe baadhi ya wanachama wa vyama vya
upinzani wamerejesha kadi za vyama vyao kikiwemo Chadema na kujiunga na
CCM kwa madai ya kuchoshwa na siasa za kutumikishwa kwa ajili ya
viongozi wa juu wa chama hicho.
Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli
ambaye hii leo hakuwa katika ubora wake kutokana na sauti yake kutotoka
vyema amewataka watanzania kumpa kura za ndio ili Tanzania iweze kupaa
kimendeleo.
Ziara ya Dr Magufuli kusaka ridhaa ya watanzania kwa ajili ya kumpa
mamlaka ya kuliongoza taifa kupitia sanduku la kura inaendelea ambapo
jumamosi ya August 29 anatarajiwa kuzungumza na watanzania wa mkoa wa
Njombe.


0 comments:
Post a Comment