Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
Mwakilishi wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua, alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
0 comments:
Post a Comment