https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    WAKALA WA KEVIN BRUYNE AELEZEA JINSI MAN CITY ILIVYOMTEKA MCHEZAJI WAKE

    2BCF937900000578-0-image-a-4_1441270794429
    Manchester City imelipa kiasi cha £54million kwa ajili ya kupata service ya mchezaji Bruyne kuanzia msimu huu.
    Wakala wa mchezaji huyu aemsema amefurahishwa jinsi Manchester city walivyokua wanam-treat mchezaji wake wakati wa kutaka kumsajili. Hapo mwanzo PSG nao pia walikua wanataka kumsajili lakini Bruyne alichagua kujiunga na Man city.
    Patrick De Koster ambae ni wakala wa Kevin alifunguka kuhusu jinsi mchezaji wake alivyopewa huduma kama movie star ,“Tulipanda ndege binafsi huko tulipotoka hadi kufika jiji Manchester. Tulipofika hapa tulipokelewa na gari la kifahari Limousines. Pia tulidhani ingekua ni kazi kubwa sana kutafuta nyumba, kufungua account, kupata simu ya nyumbani na gari. Lakini mambo yote haya yalifanyika ndani ya muda wa masaa matatu tu.”
    Unaambiwa hadi Bayern nao walikua wanamtaka mchezaji huyu lakini haikua kubwa kama kwa PSG na Man city “Tuliskia Bayern wanamtaka lakini niliwapigia simu mwenyewe na kuwambia tunataka kufanya maamuzi ya haraka ndani ya siku zilizobaki. Lakini mwisho wa siku baada ya mawasiliano mazuri na Man City niliwambia haitawezekana”
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAKALA WA KEVIN BRUYNE AELEZEA JINSI MAN CITY ILIVYOMTEKA MCHEZAJI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top