Kwa mara nyingine tena ngome ya Chelsea imeendelea kumeng’enyuka
jumamosi ya juzi baada ya kukubali kipigo cha 3-1 nyumbani kwao dhidi ya
Southampton, matokeo yanayozidi kukuza yowe la kutaka Mourinho
atimuliwe kazi.
Kipigo hicho kimewaacha mabingwa watetezi wa Premier League wakishika nafasi ya tano kutoka chini mwa msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 8 tu kutoka katika michezo 8 ya ligi.
Tuangalie matatizo makuu 6 yanayoiangusha Chelsea msimu huu.
1) Safu ya Ulinzi Inayovuja
Moja ya matatizo makubwa ya Chelsea msimu huu ni safu yao ya ulinzi, ambayo imeruhusu nyavu zao kuguswa japo mara mbili katika michezo yao ya ligi, huku Arsenal pekee iliyokuwa pungufu kwa wachezaji 9 uwanjani ndio ikishindwa kufunga goli dhidi yao msimu huu.
Kikosi hiki cha Mourinho kimesharuhusu magoli mengi katika mechi 8 kuliko ambavyo ilikuwa katika msimu wake wa kwanza wote – na ndio kwanza tupo mwezi Oktoba. Kutokuwepo kwa Thibout Courtois kunazidisha ufa kwenye safu hiyo ya ulinzi
2) Ukosefu wa Kasi kwa wachezaji/Safu ya Ulinzi
Uamuzi wa Mourinho kumuamini Kurt Zouma mbele ya Terry unatokana na kasi ya mchezaji husika.
Branislav Ivanovic amekuwa akitolewa nyongo kila wiki kwa sababu hana kasi uwanjani, hilo pia linamkuta Cesar Azpilicueta, ambaye pamoja na kuwa mzuri katika kuzuia lakini bado ni mchezaji ambaye hana kasi. Chelsea dhidi ya timu zenye mawinga wenye kasi inakuwa inapata wakati mgumu sana. Baba Rahman inabidi acheze mbele ya Ivanovi , huku Azpilicueta akihamishiwa upande wa beki ya kulia. Pea ya John Terry na Gary Cahili imegoma kuwa imara kwa sababu wachezaji wote wawili hawana kasi.
3) Uongozi
John Terry amekuwa akipoteza nafasi yake uwanjani kwa Zouma msimu huu. Zouma yupo kikosi kutoka na kasi inayoleta kwa safu ya ulinzi. Lakini bado kikosi kinaruhusu magoli. Kutokumpanga Terry hakujatibu tatizo, na kiuhalisia kutokuwepo kwa kiongozi kwenye safu ya ulinzi ndio tatizo kuu linaloikumba safu hiyo. ‘Back 4’haipo vizuri. Cahil bado hana uwezo wa Terry au kuwa na uzoefu alionao nahodha wake na labda yeye ndio alipaswa kumpisha Zouma kikosini. Bila uwepo wa Frank Lampard na Didier Drogba kikosini kunakuwa hakuna uongozi. Hili ni tatizo.
4) Matatizo ya mfumo katika staili ya uchezaji
Mfumo wa upangaji wa kikosi nao ni tatizo. Mabeki wa pembeni wa Chelsea wanapata taabu sana kwa sababu mara nyingi wanaachwa kukabiliana na upinzani wa wachezaji wawili kwa mmoja. Eden Hazard akiwa anashambulia katikati, anakuwa hawezi kurudi kushoto kuzuia, anashindwa kurudi kwenye nafasi kwa wakati. Willian nae ana tatizo kama la Hazard – akishambulia katikati anashindwa kuzuia dhidi ya beki wa kushoto wa timu pinzani. Katika mfumo wa 4-3-3 mambo yangekuwa rahisi kidogo huku Hazard akiweza kushambulia katikati na ni aina ya mchezaji ambaye anahitaji kupewa nafasi ya kushambulia katikati ili kuleta matokeo chanya zaidi.
5. Ushambuliaji
Kushuka kiwango kwa Diego Costa kumepunguza kwa kiasi kikubwa makali ya safu ya ushambuliaji. Radamel Falcao bado hajarudisha makali, lakini bado anapewa kipaumbele kwenye kikosi kuliko Loic Remy.
Magoli kutoka kwenye open play yamekauka, na vigumu kwa timu kupata zaidi ya 25% ya magoli yao kutokana na mipira iliyokufa.
6.Kutokuwa kwenye fomu kwa wachezaji muhimu
Mchezaji bora wa msimu uliopita, Eden Hazard, amekuwa kivuli cha Hazard wa msimu uliopita. Ivanovic sasa ni dhaifu mno.
Diego Costa na Cesc Fabregas nao wamekuwa vivuli vya wachezaji waliokuwa msimu uliopita.
Wachezaji waliokuwa muhimu mno katika msimu uliopita na kuiwezesha timu kubeba kombe, wote sasa wanacheza chini ya kiwango tena kwa wakati mmoja.

0 comments:
Post a Comment