Arsene Wenger ni kocha ambae amewasajili wachezaji kadhaa kutoka Monaco na wakaja Arsenal kufanya vizuri. Kabla ya Van Gaal, Arsene Wenger alishamuona Martial na kujaribu kumsajili. Wenger anasema alituma maombi kumsajili mchezaji huyo kwa Monaco lakini hakupata majibu mazuri aliyotegemea.
“Nimeshangazwa sana kuona Monaco wamemuuza Martial, pesa iliyolipwa ni nyingi najua pia unafiria hilo swala. Lakini kama wewe ungekua Monaco fikiria kiasi gani ungeweza kumuuza mwakani”
“Nilijua kwamba mwaka huu wasingeweza kumuuza kwasababu wameuza wachezaji wengi sana. Pia labda wangesimama kwenye maneno yao kwasababu nilivyojaribu kutaka kumsajili walinijibu hayupo kwenye list ya wachezaji wanaweza kuuzwa. Hivyo basi hatukuweza kuendeleza mazungumzo nae kwasababu club yake imesema hauzwi. Siku zote tulikua tunapenda aje Arsenal tangu alivyokua Lyons”


0 comments:
Post a Comment