Costa ambaye ana goli moja tu
katika michezo tisa aliyoichezea timu ya taifa ya Hispania anatumikia
adhabu ya kadi za njano na alitarajiwa kuukosa mchezo dhidi ya
Luxembourg lakini angeweza kupangwa dhidi ya Ukraine.
Spain inahitaji point moja tu
kufuzu katika michuano ya mataifa ya Ulaya na wiki ijayo itambana na
Luxembourg na Ukraine katika michezo yake ya mwisho ya kundi.
Mshambuliaji wa Juventus aliye
katika fomu hivi sasa, Alvaro Morata ameitwa kikosini na anatarajiwa
kumbadili Diego Costa katika kikosi cha kwanza.
Wachezaji wenza watatu wa Chelsea
Cesar Azzpilicueta, Cesc Fabregas na Pedro Rodriguez wote wameitwa
sambamba na Carzola wa Arsenal na wachezaji wawili wa Manchester United
David De Gea na Juan Mata huku David Silva wa Manchester City
akikamilisha orodha ya wachezaji 23.
Alipoulizwa kama tabia ya Costa
katika mechi dhidi ya Arsenal imechangia kuachwa, Del Bosque alisema,
“Hapana. Ila sikufurahishwa na tabia zake”.


0 comments:
Post a Comment