Mgombea
wa nafasi ya kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema anayeungwa mkono
na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edwrad Lowassa
ameahidi kuthibiti tatizo la mgao wa umeme ambao umekuwa changamoto
kubwa kwa wananchi.
Mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ametoa hadi hiyo
huku akionekana dhahili kuchukizwa na ahadi zisizotekelezeka za kutatua
kero hiyo ya umeme ambapo amesema serikali atakayoiunda itahakikisha
inadhibiti kikamilifu swala la mgao wa umeme.
Mgombea huyo anayeungwa mkono na asilimia kubwa ya vijana ambao ni
zaidi ya asilimia 65 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, ametumia jukwaa
hili la mkutano wa hadhara hapa Same kutoa onyo kwa shirika la umeme
nchini Tanesco.
James Mbatia mwenyekiti wa NCCR mageuzi amesema umasikini wa
watanzania unachochewa na uongozi mbovu wa CCM ambao umekuwa ukitumia
rasilimali za taifa kwa manufaa ya kundi dogo la watu wachache.
Katika siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Kilimanjaro amehutubia
mikutano ya hadhala katika maeneo ya Hedaru, Ndungu, Same na Mwanga
ambapo pia alipata fursa ya kuweka shada la maua katika kaburi la
muasisi wa CCM Peter Kisumo mjini Usangi.
0 comments:
Post a Comment