Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi
kuzindua mradi wa kusaga kokoto uliopo katika kijiji cha Pongwe Msungura
Wilayani Bagamoyo leo. Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dkt.Hussein Mwinyi, Wapili kulia, ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga,wapili kushoto ni Balozi wa Uturuki
nchini Mhe.Yasemin Eralp, watatu kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya ANIT ASFALT Bwana Semih Yaran, na wanne kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Pongwe
Msungura wakati wa ufunguzi wa mradi wa kusaga kokoto leo.
4-0843-Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi na Mkuu wa
JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaga
kokoto.kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe.Yasemin Eralp akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi wa kusaga kokoto leo.
Kikundi cha sanaa cha JKT kikitumbuiza wageni wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa kusaga kokoto.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada
ya kuwasili katika kijiji cha Pongwe Msungura kuzindua mradi wa kusaga
kokoto.Aliyesimama pembeni ya Rais ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
Meja Jenerali Raphael Muhuga. Mradi huu unaendeshwa kwa ubia kati ya
SUMA JKT na kampuni ya ANIT ASFALT ya Uturuki kwa mtaji wa shilingi
Bilioni Tano na milioni mia moja ambapo SUMAJKT inamiliki asilimia 30
sawa na shilingi Bilioni moja na milioni mia sita na themanini.
(Picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment