Watu kumi wameuwawa na wengine saba
kujeruhiwa katika tukio la mashambulizi ya risasi kwenye chuo katika
jimbo la Oregon nchini Marekani.
Polisi wamesema mtu mwenye silaha
Chris Harper-Mercer mwenye umri wa miaka 26, alifyatua risasi katika
Chuo cha Jamii cha Umpqua hapo jana asubuhi, ambapo naye aliuwawa kwa
risasi na polisi.
Kumekuwa na taarifa zinazokanganya
kuhisiana na idadi ya waliokufa katika tukio hilo hata hivyo Mkuu wa
polisi kaunti ya Dougla, John Hanlin amesema watu 10 wamekufa akiwemo
mtuhumiwa.
Mmoja wa mtu aliyepigwa risasi akiondolewa katika eneo hilo





0 comments:
Post a Comment