Arsene Wenger amenyakuwa tuzo ya Kocha bora wa Mwezi Ligi Kuu baada ya kuiongoza Arsenal kushinda mechi nne mfululizo.
Kikosi cha Wenger kiliifunga Manchester United, Watford, Everton na
Swansea City mwezi uliopita na kushika nafasi ya pili nyuma ya
Manchester City kwa tofauti ya magoli.
Arsenal ilifunga magoli 11 katika mechi nne, huku ikizinyuka 3-0 United na Swansea.
Kwa upande wa wachezaji, tuzo hiyo imeenda kwa mshambuliaji wa Leicester
City Jamie Vardy kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 15 katika klabu
hiyo.
Steven Gerrard ndiye anaongoza kwa kuzinyakua tuzo hiyo mara sita.
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Jurgen Klinsmann alikuwa wa kwanza kushinda tuzo hiyo Agosti 1994.
Wafaransa wameshinda tuzo mara 17, wapili baada ya Waingereza.
Kujua wachezaji na makocha waliowahi kunyakuwa tuzo hiyo bofya chini;
0 comments:
Post a Comment