Baadhi
ya Nyumba zikibomolewa mapema leo mchana mtaa Bwawani Manispaa ya
Kinondoni,ambapo zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali katika
Manispaa hiyo. Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa
sera ya Taifa ya Ardhi, imekusudia kuanza kuendesha zoezi la kubomoa
nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Askari
wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati
wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
mapema leo.
Baadhi
ya wakaazi wa mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni wakishuhudia bomoa
bomoa inayofanyika leo katika manispaa hiyo maeneo mbali mbali ambapo
Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya
Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila
kufuata taratibu za ujenzi.
Askari
wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati
wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
mapema leo.
Moja ya Nyumba iliyojengwa eneo la wazi katika mtaa wa Bwawani ikibomolewa
Askari jeshi la polisi wakihakikisha suala la usalama katika tukio hilo
Ubomoaji wa nyumba ukiendelea eneo la Manispaa ya Kinondoni
TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA KUHUSIANA NA UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI
Manispaa
ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi,
inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata
taratibu za ujenzi.
Maeneo
yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya
wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara
hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha
umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i.
Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa
shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa
ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.
Sera
ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na
Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
a) Bila kibali cha ujenzi
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi
hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya
Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha
zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo
ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji
huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii
inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015
hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.
0 comments:
Post a Comment