https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA LEO MUHIMBILI BAADA YA RAIS DK MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA GHAFLA


    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital
    Rais Dk. Magufuli akitokea katika ofisi ya Mkurugenzi wa MOI.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital

    Rais Dk. Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa MOI.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital

    Wananchi wakiwemo wauguzi wakishangilia ujio wa Rais Dk. Magufuli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital

    …Akimpa pole mama huyu aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital

    Rais Magufuli akimsikiliza mmoja wa wauguzi.

    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital
    Ulinzi ukiwa umeimarishwa.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital


    Msafara wa Rais Magufuli ukiondoka Muhimbili.
    Dk. John Pombe Magufuli in Muhimbili Hospital

    Wananchi wakisindikiza msafara wa Rais Magufuli.

    Na. Mwandish Wetu, Dar es Salamm.
    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

    Ujio huo wa ghafla umewafurahisha mamia ya wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo pamoja na wale wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) walioanza kuimba “hapa kazi tu”.

    Mmoja wa wagonjwa kutoka MOI aliyejitambulisha kwa jina la Chacha amesema wamepata faraja kubwa baada ya kumuona kiongozi huyo akifika hospitalini hapo.

    “Tunampongeza na tunamuombea kila heri katika utendaji wake wa kazi maana ndani ya hospitali hii kuna kero nyingi zinazowakabili wagonjwa waliolazwa wodini,” alisema Chacha.

    Rais Magufuli amesema ziara hiyo haikuwa rasmi lakini amejionea kila kitu alipotembea wodi za Mwaisela, Sewa Haji huku akijitahidi kusalimiana na kila mgonjwa.

    Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

    (HABARI/PICHA: HARUNI SANCHAWA / GPL)
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA LEO MUHIMBILI BAADA YA RAIS DK MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA GHAFLA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top