Askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu (pichani)ameeleza kushangazwa na kusikitishwa na vitendo vya mataifa makubwa duniani kuhubiri amani duniani wakati wao ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha za kivita na kuuza ili watu waendelee kupigana matokeo yake kusababisha vifo,mateso na mahangaiko katika mataifa huku wahanga wakubwa wakiwa ni watoto,akina mama na wazee.
Askofu Sangau ameyasema hayo leo asubuhi
katika adhimisho la misa takatifu ya Krismasi iliyofanyika katika
kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.
Amesema wakati dunia inaadhimisha
sikukuu ya Krismasi mataifa mengi hayana amani vita kutokana na baadhi
watu kuwa na uchu wa madaraka na fedha.
“Mataifa makubwa yanayohubiri amani
ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha, wanauza wapi? ili
upate soko la silaha,lazima utengeneze vita,watu wapigane,ili bidhaa
itoke,lakini ndiyo hao wanaokaa mezani na kusema wanataka amani,,nadhani
hawajanuia kuleta amani,uchu wa madaraka na fedha ndicho
kinachosumbua",ameeleza askofu Sangu.
"Tuwaombee wenzetu katika nchi zenye
vita,mwenyezi mungu apate kuwajalia amani na utulivu ili sote kama
familia ya watoto wa mungu tufike kule kristo ametutangulia”,ameongeza
Askofu Sangu.
Katika hatua nyingine Askofu Sangu
amewataka kuwapuuza watu wanaosema nchi ya Tanzania haina amani na
kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani huku akiwataka watanzania
kumwombea rais John Pombe Magufuli aliyeonesha nia ya kuwatumikia
wananchi bila upendeleo na ameonesha wazi wazi kuwa ana mtanguliza
mwenyezi mungu katika maisha yake.
“Kuna baadhi ya watu wanataka
kutusadikisha kuwa Tanzania hakuna amani kwa nia zao wenyewe,labda
wakilinganisha Tanzania na mbinguni ni sawa, kwa sababu mbinguni kuna
utumilifu wake wote,lakini ukilinganisha Tanzania na mataifa
mengine,ndugu zangu tuna amani ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu
zote”,ameeleza Sangu.
Katika hatua nyingine amewashangaa
wazazi na walezi wanaoruhusu watoto wao kwenda kwenye kumbi za starehe
na kusisitiza kuwa familia yoyote bora kamwe haiwezi kuruhusu mtoto
kwenda disko.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment