Michezo ya kuhitimisha hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea tena usiku wa December 9 kwa kupigwa mechi nane baada ya usiku wa December 8 kupigwa michezo nane ya Kundi A, B, C na D ila December 9 imechezwa michezo nane ya Kundi E, F, G na H,
michezo hiyo ilichezwa wakati timu 10 kati ya 32 zikiwa
zimeshajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya 16 bora hivyo nafasi 6
pekee ndio zilikuwa zinawaniwa.
Klabu ya Arsenal ambayo ilikuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi F, nafasi yake ya kuendelea hatua ya 16 bora ilikuwa mikononi mwake yenyewe, kwani ilitakiwa kuifunga Olympiakos ya Ugiriki kwa idadi nzuri ya magoli ili iweze kufuzu hatua ya 16 kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, kwani Olympiakos walikuwa wanahitaji suluhu tu ili wafuzu. Hata hivyo Arsenal ilifanikiwa kufuzu baada ya kuifunga Olympiakos kwa jumla ya goli 3-0.
Arsenal ikiwa katika uwanja wa Stadio Georgios Karaiskaki ilipata magoli yake matatu yote kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu hiyo Oliver Giroud, staa huyo aliyeipeleka Arsenal
hatua ya 16 bora alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 29, kipindi
cha pili akamalizia kwa kupachika magoli mawili dakika ya 49 na dakika
ya 67 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Olympiakos kushika mpira katika eneo la 18.
Hii ndio list ya timu zilizofuzu hatua ya 16: Real Madrid, PSG, VfL Wolfsburg, PSV Eindhoven, Atletico Madrid, Benfica, Man City, Juventus, FC Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kiev, Zenit St P na KAA Gent.
Matokeo ya mechi nyingine za UEFA za December 9
Kundi E
Kundi FKundi G
Kundi H
Video za magoli ya Olympiacos Vs Arsenal
0 comments:
Post a Comment