Kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal tayari anaonekana kukosa raha juu ya headlines za maisha yake ndani ya Man United, licha ya kuwa ni tetesi kuhusu koch huyo kuwa hatiani kufukuzwa, ila kuna kila dadlili ya uongozi wa Man United kumfuta kazi wakati wowote kuanzia sasa na nafasi yake kupewa Jose Mourinho.
Kufuatia tetesi zilizotawala na maswali machache ya waandishi vilimfanya Van Gaal kuwa wazi na kukiri kuwa tayari anajihisi kama kishafukuzwa kazi na nafasi yake kapewa Mourinho. Hizi ndio sentensi za Van Gaal baada ya kuongea na waandishi wa habari kwa chini ya dakika 5 katika mkutano na waandishi kuelekea mechi dhidi ya Stoke City.
“Kitu
kinachonishangaza ni kuwa hakuna mtu yoyote humu ndani anayejihisi
kuniomba msamaha? nafikiri mimi tayari nilishafukuzwa kazi, kocha
mwenzangu (Mourinho) tayri yupo hapa. Unafikiri nini kitatokea kwa
marafiki na familia yangu? unafikiri nataka kuongea na vyombo vya habari
kwa sasa? kiukweli nipo hapa kwa sababu ya sheria za Ligi Kuu tu, ndio
maana nalazimika kuongea” >>> Louis van Gaal
Hata hivyo Van Gaal anaonekana tayari kashakata tamaa ya kuendelea kukitumikia kikosi cha Man United,
kwani hata wakati anaondoka aliwatakiwa waandishi kheri ya sikukuu ya
Chrismass, kuhusu sikukuu ya mwaka mpya alisema labda kama tutaonana
tena, kitu ambacho kinaashiria kuwa maisha yake ndani ya Man United hayana zaidi ya wiki moja.
Hii ndio Video ya Louis van Gaal akiongea kwa huzuni katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi dhidi ya Stoke City.
0 comments:
Post a Comment