Preetha Reddy, Makamu Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo,
Na Mwandishi Wetu,
CHENNAI
ni jiji la tano kwa ukubwa nchini India, jiji hilo limepigwa na janga
kubwa la mafuriko ambayo hayajawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 100
iliyopita, mafuriko hayo yameliacha jiji hilo likiwa hoi na taabani.
Mafuriko
hayo ya kihistoria yalisababisha jiji hilo kukosa huduma muhimu kama
umeme, maji safi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi. Idadi
ya wagonjwa wengi wameripotiwa kufariki baada ya maji ya mvua kubwa
kuharibu majenereta na mfumo mzima wa umeme kwenye hospitali mbalimbali
mjini humo.
Kufuatia
mafuriko hayo makubwa jiji Chennai, hospitali za Apollo zilizopo
Chennai zimeripotiwa kuwa zinaendelea kufanya kazi vizuri na kuwa mstari
wa mbele kutoa huduma kwa waathirika wote wa hayo mafuriko. Wakati
hospitali nyingi Chennai zikiwa zinasumbuka na tatizo la umeme;
hospitali za Apollo zina endelea kutoa huduma bora na kuzidi kutumia
timu yao ya wataalamu waliojikita katika kuokoa maisha ya watu wengi.
Preetha
Reddy, Makamu Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo, alisema wametenga timu
30 zenye wataalamu wa afya kama 300 katika kukabiliana na wahanga hao
wa mafuriko.
Kwa
mujibu wa N. Sathyabhama, mkurugenzi wa huduma za afya na ubora wa kanda
ya kaskazini katika hospitali za Apollo; hospitali ya Apollo imepokea
wagonjwa wengi kutoka hospitali nyingine nyingi mbalimbali zilizokumbwa
na ukatikaji wa umeme kutokana na mafuriko.
Mwendelezo
wa huduma kutoka hospitali za Apollo katika sehemu mbalimbali jijini
umesababisha wagonjwa kutohamishiwia hospitali nyingine, licha ya
kupokea zaidi ya wagonjwa 50 ambao wengine ni wageni nchini India kutoka
hospitali nyingine zilizoathirika na janga hilo, alisema.
Wagonjwa
ambao ni wageni nchini India kutoka nchi zaidi ya 20 waliokuwepo
hospitali za Apollo walipewa kadi ya mawasialiano ya ISD na huduma ya
mtandao ili waweze kuwasialiana na familia zao, alisema Dk. Srinidhi
Chidambaram makamu wa Rais wa idara ya wagonjwa kutoka mataifa
mbalimbali. Ndugu Ahmed Noumani kutokea Oman amedhibitisha kuwa ameona
ubinadamu wa ukweli kutoka hospitali za Apollo, alijisikia yupo salama
na mwenye ulinzi mzuri na pia kuwezeshwa kuwasiliana na familia yake
muda wote iliyopo nchi ya Oman.
Ongezeko
kubwa la kiwango cha maji kwenye mabwawa ilipelekea mto Adyar kufurika
na kuleta majanga jijini na vijijini. Alisema umeme ulikatika kwa muda
wa masaa 57 katika jengo moja na masaa 69 jengo lingine lakini
waliendelea kufanya kazi kwa kutumia jenereta. Kwa ajili ya usalama,
umeme ulikatwa kwa siku kadhaa jijini Chennai na maeneo ya jirani yake.
“Tunatoa
kipaumbele katika huduma kwa wagonjwa. Ni yale matibabu ya dharura tu
na matumizi ya vifaa vya uokoaji ndivyo tulivyoshungulika navyo.
Kipaumbele kilikuwepo zaidi katika maeneo yaliyoathirika sana,” alisema
Bi. Sathyabhama
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, ukatikaji wa umeme ulifanyika kuanzia Ijumaa wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama.
Kufuatia
mvua kali zinazoambatana na upepo nchini India katika mji wa Tamil
Nadu, hospitali za Apollo zimetoa huduma bure za afya na kuweka vituo na
kambi za matibabu kwa wahanga wote jijini Chennai.
Kambi
iliwekwa katika ofisi ya baraza kuanzia saa tatu asubuhi. Timu ya
madkatari 20 inayojumuisha wataalamu wa magonjwa ya tumbo
(gastroenterologists), madaktari wa kawaida, wataalamu wa magonjwa ya
watoto (paediatricians),wataalamu wa magonjwa ya wanawake
(gynaecologists), wataalamu magonjwa ya shingo na kichwa (ENT
specialists),wataalamu wa uti wa mgongo na misuli (orthopaedicians), na
wataalamu wa magonjwa ya mapafu (pulmonologists) wakiwa na manesi 20 na
matabibu wengine kutoka Hospitali za Apollo waliwekwa kwenye hizo kambi.
Hospitali
za Apollo zimetoa mchango mkubwa sana katika kuokoa maisha ya wananchi
wengi wa India katika kipindi hiki cha mvua za mafuriko jijini Chennai.
Magwiji hao wanaongoza kwa huduma bora za afya ulimwenguni wameonyesha
mfano wa kuigwa wa namna vituo vya afya vinatakiwa kuwa bora na msaada
katika kuokoa maisha hasa pale majanga yanapoteka
0 comments:
Post a Comment