Nehemiah
Mchechu, moja ya majina maarufu katika nyanja za uongozi wa mashirika
nchini, jina lake limeteka mitandao ya kijamii kwa zaidi ya mwezi mmoja
sasa.
Ukiachana
na umaarufu wa Rais John Magufuli mtandaoni kwa kazi yake ya ‘kutumbua’
majipu, Mchechu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania
(NHC), anavuma kwa mema na ‘mabaya’.
Baadhi
wanasifu mafanikio yake ya kuliimarisha shirika hilo kwa kipindi cha
muda mfupi, lakini wengine wanamtuhumu kulitumia kujinufaisha ikiwamo
kujilipa ‘mamilioni’ ya shilingi kama mshahara na posho za vikao.
Tuhuma
zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba bosi huyo wa NHC,
anajilipa mshahara Sh36 milioni kwa mwezi na kuhudhuria vikao vingi vya
bodi vinampatia posho za kutisha.
“Kiwango hicho hakina ukweli,” anasema Mchechu, “mshahara wangu upo chini ya hapo,”anasema.
“Pia, huwezi kujilipa. Unalipwa kwa makubaliano maalumu tangu awali kabla ya kazi kulingana na kazi unayopewa,” anaongeza.
Mchechu
anasema yupo NHC kulitumikia taifa kwa kuwa alipotoka sekta binafsi
alikuwa akipata mshahara mkubwa, lakini alikubali kiwango kidogo
serikalini kwa kuwa alikuwa akijua shirika hilo lilikuwa na hali mbaya
kifedha na lilihitaji kuboreshwa.
Kuhusu
vikao vya bodi na kamati mbalimbali anazotuhumiwa kushiriki na ‘kuvuna
fedha’, Mchechu anasema kamati nyingi zinazorushwa mtandaoni siyo za
kweli na hakuna fedha inayolipwa katika vikao hivyo.
“Watu
wanapohoji mshahara wangu wanasahau kiwango ninachoingiza kwa Serikali.
Jaribu kufikiri tumeirudisha ardhi ya Kawe Tanganyika Parkers yenye
thamani ya zaidi ya Sh200 bilioni kutoka mikononi mwa aliyekuwa ameuziwa
kipindi hicho, hivi ningekuwa mtu binafsi kwa kufanikisha majadiliano
ya kurudisha kiwanja hicho, ningepata kiasi gani?” anasema.
Katika
mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni, Mchechu anaeleza kuwa
Watanzania ni kigeugeu kwa kuwa wakati anaingia NHC mwaka 2010 akitokea
Benki ya CBA, wengi walimuonea huruma wakieleza alikuwa anakwenda
kupoteza weledi na mshahara, lakini sasa wanamzushia anapokea fedha
nyingi zinazolifilisi shirika.
“Siku
waajiri wangu wakigundua nalipwa mshahara mkubwa kuliko ninachofakifanya
wataniondoa kwa sababu nawaletea hasara,” anasema.
Bosi
huyo wa zamani wa Benki ya Standard Chartered alianza kazi mwaka 2010,
wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kupatiwa mkataba wa miaka
minne kuboresha shirika hilo lililokuwa likichechemea.
Mkataba wa awali ulimalizika mwaka jana na kusaini mwingine wa miaka mitano ambao unatarajia kumalizika mwaka 2018/2019.
Kama
yalivyokuwa malengo ya Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962, Mchechu,
alikabidhiwa kazi ya kuendeleza sera ya kujenga makazi ya bei nafuu kwa
Watanzania.
Kama
ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya umma, NHC halikuwa likipata faida
kubwa ya kuwezesha kuendeleza miradi mikubwa na kwa mujibu ripoti za
fedha za shirika hilo, mwaka 2010 lilikuwa limepata faida ya Sh3.1
bilioni.
Ili kulifanyia mabadiliko Shirika hilo, Mchechu anasema, ilihitajika
akili na nguvu ya kutosha kwa sababu mambo yalikuwa yakiendeshwa
kienyeji na kwamba baadhi ya vigogo walikuwa wakihusika kulifilisi NHC.
Mikataba ya vigogo
Anasema
kuwa kuna baadhi ya vigogo serikalini na watumishi wa shirika hilo
waliokuwa wakiendesha ukodishaji wa nyumba kwa mikataba ya kilaghai na
NHC kwa kulipatia fedha kidogo wakati wanatoza fedha nyingi kwa
wapangaji.
Kuna
baadhi ya ‘madalali’ walikuwa wakililipa shirika kodi ya Sh700, 000
katika baadhi ya nyumba za biashara kwa mwezi wakati wao wanakusanya
zaidi ya Sh5 milioni lakini mikataba hiyo ilivunjwa.
“Tumekirejesha
alichokuwa akikitaka Baba wa Taifa kwa sababu kwa sasa karibu kila mkoa
una nyumba za bei nafuu zilizojengwa na shirika,” anasema Mchechu
akieleza kuwa hadi sasa wamejenga nyumba zaidi ya 3,000 za bei ya chini.
Katika
mtandao wa nyumba hizo, zilizokuwa zikiuzwa bei ya chini kuliko zote
nchini ni zile zilizopo mkoani Katavi ambazo zilikuwa Sh32 milioni kwa
sababu huduma za umeme na barabara zilikuwa zimesogezwa.
Anaeleza
kuwa wastani wa bei ya makazi ya bei nafuu ni Sh34 milioni kwa nyumba
ya vyumba viwili na Sh43 milioni kwa nyumba ya vyumba vitatu na bei
hupanda kutokana na gharama za ujenzi zikiwamo kuandaa miundombinu na
kodi ya ongezeko la thamani.
Pia,
gharama hizo anasema zinatokana na riba kubwa ya mikopo iliyopo sokoni
na kupanda kwa thamani ya Dola ya Marekani mara kwa mara.
Hata
hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema nyumba hizo zinauzwa ghali na
kununuliwa na mabepari pekee badala ya walengwa ambao ni watu wa kipato
cha chini na sehemu kubwa zinadoda kwa kukosa wateja.
Kwa Mchechu, tuhuma hizo hazimnyimi usingizi. Na kabla ya kujibu hoja hiyo, anatasabasamu kidogo.
“Kila
mradi tunaoufanya huwa tunalenga watu wa kundi fulani. Hatukurupuki.
Tunaangalia wa kipato cha chini, kati na cha juu. Sina sababu ya
kuficha.
“Lakini
nyumba zetu ni za bei ya chini kulinganisha na kampuni binafsi hivyo
naomba fananisha embe kwa embe na chungwa na chungwa na si vinginevyo,”
anasema.
Mchechu
anasema kuna baadhi ya miradi mikubwa kama ya Kawe na Morocco ni ya
kibiashara zaidi na nyumba zake zinauzwa bei kubwa kwa kuwa zililenga
kundi la watu ambao hukimbilia nje ya nchi kununua makazi lakini sasa
wanataka wabaki nchini.
“Kama
mtu ni wa malengo ya Sh50 milioni halafu anakosoa bei za mradi wa Kawe
yupo sahihi kuona bei ile ni kichaa kwa sababu inaenda mara tatu hadi 10
ya kipato chake. Lakini mimi sikulenga kule,” anasema.
Nyumba za bei nafuu
Hata
hivyo, anaeleza kwa kuwa NHC malengo yake ni kujenga nyumba za bei nafuu
katika halmashauri zote nchini ambako tayari wamenunua ekari 5,600 huku
nyingine 22,000 wapo kwenye mazungumzo ya kuuziana na wamiliki.
Kuhusu kudoda kwa nyumba, bosi huyo anapinga kidogo.
Anasema
makazi mengi waliyoyajenga kwa bei nafuu yalinunuliwa yote na mengine
kabla ya miradi yake kukamilika kupitia mikopo ambayo wananchi wanakopa
benki za biashara kununua nyumba za NHC.
“Kibada,
Kigamboni (Dar es Salaam) tuliuza ndani ya saa 48, mradi wa Eco Housing
na Mchikichini zote zimeuzwa hata hizo za mikoani zina soko…hakuna
zilizododa,” anasema Mchechu.
NHC
inafahamika kwa muda mrefu kuwa na nyumba za kupangisha za bei nafuu
nchini lakini kwa sasa miradi yake ya kupangisha haisikiki kwa kiasi
kikubwa.
Hata hivyo, majibu ya kiongozi huyo yanashitua kidogo kwa wanasubiri kiwango kikubwa cha nyumba za kupangisha.
Anasema
kuwa katika mikakati yao walipanga kujenga nyumba asilimia 70 kwa ajili
ya kuuza na asilimia 30 ya kupangisha kwa watu wa hali ya chini.
Matangazo ya ukodishaji hayawi makubwa sana kama ilivyo katika uuzaji kwa kuwa wananchi wengi wanahitaji nyumba hizo, anaeleza.
“Tanzania
ina upungufu mkubwa wa nyumba takriban 3.5 milioni hivyo iwapo nikisema
nijenge nyumba moja kwa Sh100 milioni na kuikodisha ile fedha itasaidia
familia moja tu lakini nikiuza nyumba mtaji ule nikauzungusha tunaweza
kujenga zaidi ya nyumba nane za familia,” anasema Mchechu.
Tangu
Rais John Magufuli aingie madarakani ameanza kubadilisha utendaji kwenye
utumishi wa umma na moja ya njia ya kufanikisha hilo ni ziara za
kushtukiza katika taasisi na mashirika ya umma.
Mchechu amejiandaje na ujio wa kushtukiza wa Rais?
“Sisi tayari tulikuwa tunaendesha mambo yetu kwa mwendokasi na baadaye tutaongeza zaidi kasi,” anasema.
Katika
uongozi wake, anaeleza aliyoyapata NHC yakiwamo kuongeza uwekezaji wa
ujenzi nyumba nchini na kukuza mapato ya shirika ambayo mwaka jana
yalifikia Sh130 bilioni kutoka Sh36.6 bilioni mwaka 2010 baada ya kubana
matumizi na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.
“Pesa
tumeikuza lakini haitosheelezi miradi hata ukichanganya na mikopo hivyo
tunaendelea kutafuta fedha zaidi ili kufanikisha malengo yetu.
“Na
pia niwe muwazi kabisa kama nitashindwa kutimiza malengo kwa miaka tisa
niliyokaa NHC sidhani kama nitaleta kipya nikipatiwa miaka 20 hivyo
baada ya hapa nitarudi sekta binafsi,” anasema.
0 comments:
Post a Comment