Mmoja wa wakuu wa kanisa katoliki amesema kuwa mpango wa uzazi unaweza ''kutoa suluhu'' ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Kardinali
Peter Turkson, ambae ni mshauri mkuu wa Papa Francis wa masuala ya hali
ya hewa, ameiambia BBC kuwa kanisa halijawahi kupinga mpango wa uzazi
wa njia asilia.Akizungumza mjini Paris, Kardinari huyo alittoa wito wa kuwepo kwa makubaliano thabiti yatakayolinda nchi zinazoathirika zaidi.
Anasema mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha maafa makubwa kwa viumbe hai.
Cardinal Turkson anaaminiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuandaa muswada wa Papa Francis wa mabadiliko ya hali ya hewa al maarufu "Laudato Si".
Hivi karibuni kanisa katoliki liliidhinisha ushiriki wake mkubwa katika suala la mazingira, likiwahamasisha waumini kushiriki matembezi ya dunia kuhusu uhifadhi wa mazingira kabla ya kuanza kwa mkutano wa dunia wa Mazingira COP21.
Kanisa katoliki ia limeongeza ushiriki wake katika mchakato wa mazungumzo yanayohusu masuala ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment